WASICHANA TUMBI SEKONDARI WAMPA HESHIMA RAIS SAMIA

Esther Kilamwegula msichana pekee aliyepata daraja la kwanza alama ya nane kutoka shule ya Sekondari Tumbi Kibaha Na. Gustafu Haule,Pwani WANAFUNZI wakike 34 waliofanya mtihani wa kumaliza kidato cha nne mwaka 2023 katika Shule ya Sekondari ya Wananchi Tumbi iliyopo Halmashauri ya Mji Kibaha wamempa heshima Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuonyesha maajabu makubwa ya ufaulu. Maajabu hayo yametokea kwa mara ya kwanza katika Shule ya Kata Sekondari Tumbi kwa kuhakikisha wanafunzi wote wakike waliofanya mtihani huo kufaulu kwa kiwango cha juu jambo ambalo limepelekea Shule hiyo kufanya vizuri kwa Mkoa wa Pwani. Ufaulu wa wanafunzi hao wa kike ni heshima kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Makamu wa Rais Dkt.Philipo Mpango ambaye mwaka jana alitoa motisha ya Sh.milioni 50 Kwa walimu wa Shule hiyo baada ya kupokea ripoti ya matokeo mazuri ya ufaulu shuleni hapo. Mkuu wa Shule ya Sekondari ya ...