WASICHANA TUMBI SEKONDARI WAMPA HESHIMA RAIS SAMIA

Maajabu hayo yametokea kwa mara ya kwanza katika Shule ya Kata Sekondari Tumbi kwa kuhakikisha wanafunzi wote wakike waliofanya mtihani huo kufaulu kwa kiwango cha juu jambo ambalo limepelekea Shule hiyo kufanya vizuri kwa Mkoa wa Pwani.
Ufaulu wa wanafunzi hao wa kike ni
heshima kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Makamu wa Rais
Dkt.Philipo Mpango ambaye mwaka jana alitoa motisha ya Sh.milioni 50 Kwa
walimu wa Shule hiyo baada ya kupokea ripoti ya matokeo mazuri ya ufaulu
shuleni hapo.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Tumbi Fidelis Haule,akizungumza na waandishi wa habari shuleni hapo jana amesema kuwa Shule yake inajivunia kuona wanafunzi wote wakike waliosoma shuleni hapo wamefaulu kwa kiwango cha juu jambo ambalo kwake ni faraja.
"Ufaulu wa wanafunzi wa kike katika Shule yetu imefikia asilimia 99 kwakuwa wote wamepata ufaulu wa juu na sisi kama Shule tunajivunia kuwa na matokeo haya ambayo yameleta heshima kwa mama yetu Rais Samia Suluhu Hassan,"amesema Haule
Amesema kuwa,siri ya wanafunzi hao kufaulu imetokana na nidhamu nzuri inayotekelezwa na walimu pamoja na wanafunzi wa kike ,motisha kwa walimu ,utambuzi kwa wanafunzi wanaofanya vizuri na hata kuweka malengo katika ufundishaji.
"Sisi hapa shuleni kwetu tuna utaratibu wa kila mwaka wa kutoa pongezi kwa walimu wanaofanya vizuri katika masomo yao na huwa tunawapa vyeti lakini kwa wanafunzi wanaofanya vizuri pia tunawapa vyeti mbele ya wenzao ili kuwapa moyo wa kusoma kwa bidii,"amesema Haule
Haule,ameishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwani imetoa fedha nyingi kwa ajili ya kukarabati miundombinu ya Shule ikiwemo kujenga maabara,kuboresha madarasa, kuongeza viti na vifaa vya ufundishaji na kikubwa walichopanga na kulipa fadhila kwa Rais kwa kuhakikisha kila mwanafunzi wakike anafaulu vizuri

"Rais mama Samia ametuletea kila kitu,yaani majengo mazuri,walimu wakutosha kwahiyo tunakila sababu ya kumshukuru na ndio maana tukasema lazima tuhakikishe tunalipa fadhila na tumefanikiwa kwani wasichana wote wamefaulu tena kwa kiwango cha juu,",amesema Haule
Mkuu huyo amesema mikakati ya Shule yake ni kuongeza juhudi na maarifa katika ufundishaji ili kuhakikisha wanafunzi wanaomaliza kidato cha nne wanakuwa na matokeo mazuri zaidi na kwamba wanachohitaji ni kuona wanafunzi wakike wanazidi kuwa vinara katika ufaulu ili kuendelea kuunga mkono jitihada za Rais Samia katika kuboresha mazingira ya elimu hapa nchini.
Kufuatia matokeo hayo mapema jana Haule ametoa zawadi ya pesa kwa mwanafunzi wakike aliyefanya vizuri katika mtihani huo Esther Kilamwegula huku akiwataka wanafunzi wa kidato cha nne wanaotarajia kufanya mitihani yao mwaka huu kuongeza jitihada katika masomo ili waweze kufaulu vizuri zaidi.
Kwa upande wake Esther Kilamwegula ambaye kinara wa matokeo ya kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Tumbi ,amesema kuwa watu wanafikiri sio rahisi kwa Shule za Kata kufaulisha kwa alama za juu lakini kwa Shule ya Sekondari Tumbi imewezekana.
Comments
Post a Comment