BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJINI LAMPONGEZA MKURUGENZI WAKE KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA SAMBAMBA NA KUONGEZA MAPATO.



Na Gustaphu Haule,Pwani

BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Mji Kibaha limempongeza mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Dkt.Rogers Shemwelekwa kwa usimamizi mzuri katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Shemwelekwa ameshushiwa pongezi hizo Aprili 29, 2025 katika kikao cha Baraza hilo kilichofanyika katika Ukumbi wa soko kubwa la kisasa (Kibaha Shopping Mall) ambapo kwa kiasi kikubwa lilikuwa Baraza za kuonyesha mafanikio katika kipindi cha mwaka 2020/2025.


Pongezi hizo zilikuja mara baada ya Wenyeviti wa kamati mbalimbali ikiwemo kamati ya fedha, kamati ya Mipango Miji, kamati ya Afya na Elimu pamoja na kamati ya huduma za jamii kueleza mafanikio ndani ya kipindi hicho cha miaka mitano.

Mwenyekiti wa kamati ya fedha Karim Ntambo,amesema kuwa katika kipindi cha miaka mitano Manispaa ya Kibaha Mjini imepata mafanikio makubwa ambapo moja ya mafanikio hayo ni pamoja na ongezeko la mapato.



Ntambo, amesema kuwa wakati wanaingia madarakani ukusanyaji mapato ulikuwa ni kiasi cha Sh.bilioni 4 lakini ikaongezeka mpaka kufikia Sh.bilioni 8 na tangu mkurugenzi huyo aingie Kibaha mambo yameanza kubadilika na mapato ya Halmashauri yamezidi kuongezeka zaidi.

Amesema mafanikio hayo yametokana na ushirikiano baina ya mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Dkt.Rogers Shemwelekwa ,Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka pamoja na Madiwani hao.

Nae Mwenyekiti wa kamati ya afya na elimu ambaye pia ni diwani wa Kata ya Visiga Kambi Legeza,amesema kuwa katika kipindi chao Halmashauri imefanikiwa kupata vituo vya afya viwili.

Legeza, amesema kuwa mbali na vituo hivyo lakini pia Halmashauri imejenga Zahanati tisa, ukarabati wa kituo cha afya Mkoani na kuongeza vifaa tiba ambapo fedha zake zimetoka Serikali Kuu, Halmashauri pamoja na nguvu za Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka.

Kutokana na mafanikio yalitajwa na mengine mengi yaliyofanyika katika Halmashauri hiyo madiwani hao hawakusita kumpongeza mkurugenzi huyo kwa kazi kubwa aliyoifanya huku wakimtaka kuendelea kuchapakazi Kwa maslahi ya Wananchi wa Kibaha Mjini.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kibaha Mjini Musa Ndomba, amesema kuwa mkurugenzi huyo toka aingie katika Halmashauri hiyo ameleta mabadiliko makubwa ya kimaendeleo na amekuwa msimamizi mzuri wa utekelezaji wa miradi.

"Baraza hili kwa pamoja tunampongeza mkurugenzi huyu Shemwelekwa na timu yake kwa kazi nzuri aliyoifanya hasa katika kuwezesha utekelezaji wa ilani ya CCM pamoja na ukusanyaji wa mapato ndio maana leo hii Kibaha Mjini imepandishwa hadhi na kuwa Manispaa,"amesema Ndomba 

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kibaha Mjini Mwajuma Nyamka,amemshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuiwezesha Kibaha Mjini kupata maendeleo makubwa kwakuwa mafanikio ya Kibaha yametokana na Rais kutoa fedha kwa wakati.

Pamoja na hayo lakini pia Nyamka aliweka bayana pongezi zake kwa Halmashauri ya Mji Kibaha chini ya mkurugenzi huyo kwakuwa miradi mingi imetekelezwa kwa mapato ya ndani .

",Najua mafanikio ya Kibaha Mjini yametokana na ushirikiano wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, Mbunge Koka,na Madiwani lakini nimeona tangu mkurugenzi ateuliwe kuletwa hapa mambo yamekuwa mazuri zaidi,",amesema Nyamka 

 Nyamka ametaka miradi ya yote ya Kimkakati lazima izingatie maslahi mapana ya pande zote ikiwemo Halmashauri,Serikali na CCM kwakuwa Chama hicho ndio msimamizi wa utekelezaji wa ilani.

Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Dkt.Rogers Shemwelekwa amemshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kumteua kuwa mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha na kwamba anachofanya ni kuonyesha imani juu ya uteuzi wake.



Hatahivyo, pamoja na mafanikio yaliyopatikana Dkt.Shemwelekwa ameahidi kuendelea kufanyakazi kikamilifu kwa ajili ya kusukuma gurudumu la maendeleo zaidi.

Mwisho.


Club News Editor

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

RC PWANI AONGOZA WAKAZI PWANI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA

RAIS SAMIA ATANGAZA KIBAHA MJINI KUWA MANISAPAA,MBUNGE KOKA AFURAHIA ASEMA KIBAHA ITANG'AA