RC PWANI AFURAHISHWA NA UTENDAJI KAZI WA MKURUGENZI WA KIBAHA MJINI DKT.ROGERS SHEMWELEKWA



Na Gustaphu Haule,Pwani 

MKUU wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge,amelipongeza Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Mji Kibaha kupitia mkurugenzi wake Dkt.Rogers Shemwelekwa kwa kazi nzuri ya kutekeleza miradi ya maendeleo iliyofanywa kwa kipindi cha mwaka 2020/2025.

Aidha, Kunenge amesisitiza Baraza hilo kuwa katika kipindi cha mwaka 2025 /2030 wahakikishe wanapanga miradi yenye kipaumbele ili kuleta matokeo chanya katika jamii.

Kunenge,ameyasema hayo Juni 16,2025 wakati akizungumza katika kikao maalum cha Baraza la Madiwani kwa ajili ya kujibu hoja za mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG)kikao ambacho kimefanyika katika Halmashauri ya Mji Kibaha.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha Musa Ndomba akizungumza katika kikao cha  Baraza maalum la kujibu hoja za mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) kilichofanyika Juni 16,2025 

Amesema kuwa Kibaha Mjini imekuwa Halmashauri ya kuigwa kwakuwa katika kipindi kifupi tangu mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Dkt.Shemwelekwa kuingia katika Halmashauri hiyo yapo mabadiliko makubwa ya kimaendeleo yamefanyika .

Amesema Kibaha Mjini imefanikiwa kutekeleza miradi mingi ya kimaendeleo ikiwa ukamilishaji wa soko la Kisasa la Kibaha Shopping Mall, ujenzi wa Shule za mchepuo wa Kiingereza pamoja na miradi mingine mbalimbali.

Kunenge, ameongeza kuwa mbali na hilo lakini pia mkurugenzi huyo na timu yake wamefanikiwa kuongeza makusanyo ya mapato ya Halmashauri kutoka Sh.bilioni 4 ya Mwaka 2023  mpaka kufikia Sh. bilioni 10 ya Mwaka 2024 huku mwaka 2025 /2026 wakitarajia kufikia mapato ya Sh.bilioni 20.

" Mimi nampongeza mkurugenzi wa Halmashauri hii ya Kibaha Mjini kwa kazi nzuri aliyoifanya kwani katika kipindi kifupi tumeona mabadiliko makubwa ya kimaendeleo na mafanikio hayo yametokana na ushirikiano mzuri na timu yake,hivyo naamini kwa kazi hii kubwa Madiwani wote watarudi,"amesema Kunenge 

Aidha, Kunenge amewasisitiza Madiwani pamoja na watumishi wa Halmashauri hiyo kutumia 4R za Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwakuwa wakifanya hivyo Halmashauri itakuwa haina vurugu .
Kwa upande mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kibaha Musa Ndomba amesema Halmashauri hiyo imefanyakazi na Wakurugenzi watatu na kila mtu alitimiza wajibu wake lakini Dkt . Rogers Shemwelekwa amekuwa mkurugenzi wa mfano zaidi kutokana na uchapakazi wake.

Ndomba , amesema ukiwa kiongozi lazima uchague vitu vya kuvifanyia kazi ili kukomesha changamoto ndogondogo zinazojitokeza sehemu ya kazi na Shemwelekwa anatambua hilo ndio maana Halmashauri imesonga mbele.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha Musa Ndomba akizungumza katika kikao cha  Baraza maalum la kujibu hoja za mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) kilichofanyika Juni 16,2025 

Amesema, katika kipindi cha miaka mitano ya Baraza hilo imeonekana limefanyakazi kubwa lakini sababu kubwa ni Rais Dkt . Samia Suluhu Hassan ambaye ameweza kuleta fedha nyingi za utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

"Baraza hili linamshukuru sana Rais wetu mama Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha nyingi hapa Kibaha lakini sio hilo tu,kwani hata alipoamua kuchukua hatua ya malipo ya  madiwani kuwa analipa yeye ni jambo kubwa sana kwakuwa ametupa heshima kubwa Madiwani wa nchini hii," amesema Ndomba.

Hatahivyo, ameiomba Serikali kuangalia upya namna ya kulipa posho za madiwani ikiwezekana ziongezeke ili kuwapa molari Madiwani hao kufanyakazi kwa bidii sambamba na kupambana na watumishi wasio waadilifu.

Mwisho.

Club News Editor

Comments

Popular posts from this blog

RC PWANI AONGOZA WAKAZI PWANI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA

BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJINI LAMPONGEZA MKURUGENZI WAKE KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA SAMBAMBA NA KUONGEZA MAPATO.

RAIS SAMIA ATANGAZA KIBAHA MJINI KUWA MANISAPAA,MBUNGE KOKA AFURAHIA ASEMA KIBAHA ITANG'AA