Posts

MADEREVA WA POLISI PWANI WATAKIWA KUWA MFANO BARABARANI

Image
Na. Julieth Ngarabali, PWANI. Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Pwani, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Edson Mwakihaba, amewataka madereva wa Jeshi la Polisi mkoani humo kuwa kioo cha jamii na mfano wa kuigwa wanapokuwa barabarani. Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Pwani, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi  (SSP) Edson Mwakihaba Mwakihaba ameyasema hayo , Agosti 14, 2026, wakati akifungua mafunzo ya siku moja kwa madereva wa magari ya polisi, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Benjamin Mkapa Polisi Mkoani Pwani. Mafunzo hayo yanalenga kuwakumbusha umuhimu wa kutii sheria za usalama barabarani bila shuruti. Amesisitiza kuwa kuwa askari polisi hakumpi dereva haki ya kuvunja sheria za barabarani. Hivyo, amewataka kuzingatia kanuni zote ikiwemo kuepuka mwendo kasi, kuheshimu taa za kuongozea magari, na kutoa kipaumbele kwenye vivuko vya watembea kwa miguu (zebra crossings). Washiriki wa Mafunzo ya Madereva wa Magari ya Polisi "Ili kufanikiwa katika mapambano dhidi ya ...

MKOA WA PWANI WATATHMINI MALEZI YA AWALI YA MTOTO: ZAIDI YA VITUO 400 VYA DCCA VIMESAJILIWA

Image
Na Julieth Ngarabali, PWANI. Mkoa wa Pwani umefanya tathmini ya utekelezaji wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM) kwa kipindi cha Januari hadi Juni 2026, kinacholenga kuimarisha ustawi na huduma kwa watoto wenye umri wa miaka 0 mpaka 8. Kwenye tathmini hiyo pamoja na mambo mbalimbali yaliyowasilishwa imeelezwa jumla ya vituo 858 vya kulelea watoto wadogo mchana (DCC) vimeainishwa, ambapo vituo 477 tayari vimesajiliwa na vinahudumia watoto 19,478—sawa na asilimia 56 ya vituo vyote vilivyotambuliwa kimkoa. Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji, Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Lidya Mafole amesema pia kuna vituo saba vya malezi ya jamii (Community ECD) vilivyoanzishwa na shirika la BRAC tangu mwaka 2025 ambavyo mchakato wa usajili wake unaendelea. Bi.  Lidya Mafole  Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mafole amebainisha kuwa katika kipindi hicho, vikao vya tathmini vimefanyika ...

TRA MKOA WA PWANI YATOA ELIMU YA MABADILIKO YA SHERIA ZA KODI 2026

Image
Na. Charles Kusaga, Kibaha - PWANI Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)  imeendesha semina ya elimu kuhusu mabadiliko ya sheria za kodi kwa mwaka 2026, iliyowakutanisha wafanyabiashara, wahasibu, watoa huduma za kodi na wadau mbalimbali katika Ukumbi wa Destiny, Kibaha Mkoa wa PWANI Lengo la semina hiyo lilikuwa kuwajengea walipakodi uelewa wa mabadiliko ya sheria za kodi, taratibu za ulipaji kodi pamoja na umuhimu wa kuzingatia sheria za kodi ili kuongeza uwajibikaji na kuchangia maendeleo ya taifa. Washiriki walipata fursa ya kuuliza maswali na kupata ufafanuzi  kuhusu changamoto mbalimbali zinazowakabili walipakodi, huku wakihimizwa kuendelea kufuata sheria na kutumia huduma za kidijitali zinazotolewa na mamlaka hiyo. TRA imeendelea kusisitiza kuwa elimu ya mlipakodi ni nyenzo muhimu katika kuongeza uelewa wa wananchi, kuboresha hiari ya ulipaji kodi na kuimarisha ushirikiano kati ya mamlaka na walipakodi. Club News Editor

MIAKA 30 YA TRA: TEKNOLOJIA NA HUDUMA BORA ZAIMARISHA UHUSIANO NA WALIPA KODI MKOA WA PWANI

Image
Na Charles Kusaga, Pwani Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika maadhimisho ya miaka 30 tangu kuanzishwa kwake tarehe 01 Julai 1996, imedhihirisha ukuaji wa huduma bora na teknolojia huku ikijivunia hatua kubwa iliyofikiwa katika kuimarisha mahusiano mema na ushirikiano thabiti na walipa kodi mkoa wa Pwani. Akizungumza na wadau mbalimbali wa kodi mkoani hapa katika ufunguzi wa kongamano la maadhimisho ya miaka 30 ya TRA kwa mkoa wa Pwani Menejea wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Ndugu Peter Eliona alizungumzia mafanikio ya Mamlaka ya Mapato nchini.  Kwa mkoa wa Pwani alieleza kuwa katika kipindi hiki cha miongo mitatu, TRA Mkoa wa Pwani imeshuhudia mabadiliko makubwa kutoka katika mifumo ya kizamani ya ukusanyaji mapato na kuingia katika ulimwengu wa kidigitali. Mabadiliko haya ya kiteknolojia yamekuwa nguzo kuu katika kurahisisha utoaji wa huduma na kuondoa urasimu uliokuwa ukiwapa changamoto wafanyabiashara na wananchi mkoani humo. Pia huduma bora, Elimu kwa wateja na ushirikia...

RC MJINI MAGHARIBI AIKARIBISHA HALMASHAURI YA MBEYA KATIKA FURSA ZA UWEKEZAJI ZANZIBAR

Image
Na Mwandishi Wetu,Zanzibar Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar, Mhe. Moh’d Ali Abdallah, ameushukuru uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kwa kufanya ziara katika Mkoa huo, akieleza kuwa hatua hiyo inafungua fursa mpya za ushirikiano wa kiuchumi kati ya pande hizo mbili. Akizungumza na viongozi hao, Mhe. Abdallah alisema Mkoa wa Mjini Magharibi uko tayari kuimarisha mahusiano ya kibiashara na Mkoa wa Mbeya, hasa katika sekta ya mazao ya kilimo. "Hii kwetu ni fursa ya kufanya biashara na Mkoa wa Mbeya. Kama mlivyopita katika masoko yetu mmeona viazi na mchele kutoka Mbeya. Karibuni muwekeze Zanzibar, tutawapa eneo maalumu na tutaandika wazi kuwa bidhaa hizo zinatoka Mbeya ili wanaohitaji mazao hayo wajue mahali pa kuyapata kwa bei ya jumla," alisema Mhe. Abdallah. Aliongeza kuwa uwekezaji huo utasaidia kuongeza upatikanaji wa mazao kutoka Mbeya katika masoko ya Mjini Magharibi huku ukiwanufaisha wakulima na wafanyabiashara wa pande zote mbili kupitia masoko ya uhakik...

RC PWANI ATAKA MRADI WA IPOSA UTOE MATOKEO CHANYA KWA VIJANA

Image
Na Gustaphu Haule, Pwani  MKUU wa Mkoa wa Pwani  Abubakar Kunenge, ameielekeza Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima kuhakikisha programu ya Mpango wa IPOSA  inakuwa na matokeo chanya kwa kuwajengea vijana uwezo wa kujiajiri na kuajirika. IPOSA ni Mpango ulioandaliwa na Taasisi ya Elimu ya Watu wazima wa elimu changamani kwa Vijana walio nje ya Shule.  Kunenge ametoa maelekezo hayo wakati akifunga mafunzo ya walimu wa programu hiyo yaliyofanyika Oktoba 2,2025 katika  ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha. Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge akizungumza na wasimamizi wa mradi wa IPOSA katika mkutano uliofanyika Oktoba 2,2025 katika ukumbi mdogo wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha. Alisema kuwa  elimu inayotolewa kupitia IPOSA haipaswi kubaki kwenye vyeti pekee, bali iwe chachu ya mabadiliko katika maisha ya vijana ambao wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya ajira. “Mradi huu wa IPOSA lazima uwe na matokeo ya kweli, vijana wanapaswa kufundish...

TISEZA YAKARIBISHA WAWEKEZAJI KWALA YATENGA EKARI 100 KWA AJILI YA UWEKEZAJI

Image
  Na Gustaphu Haule, Pwani  MAMLAKA ya Uwekezaji na Maeneo Maalumu ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) imesema imetenga ekari 100 katika eneo la Kwala katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani kwa ajili ya ujenzi wa viwanda. Kaimu Meneja Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma kutoka TISEZA Adelina Rushekya ametoa kauli hiyo Septemba 30,2025 wakati akizungumza na Waandishi wa habari katika mkutano maalum uliofanyika eneo la Kwala. Kaimu meneja Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma kutoka TISEZA Adelina Rushekya akizungumza na Waandishi wa habari katika eneo la Kwala. Rushekya amesema kuwa maeneo ya Kwala yana vivutio vinavyotakiwa kwa ajili ya uwekezaji huku akisema fursa za uwekezaji zipo vizuri katika kila sekta. Rushekya amesema mwekezaji atakayekuwa tayari kuwekeza katika eneo hilo atapatiwa ekari moja na pia anatakiwa kuwa na mtaji wa dola za Kimarekani milioni tano kwa wazawa na kwa raia wa kigeni anatakiwa kuwa na dola milion kumi. Aidha Rushekya amesema kuwa  mwekezaji at...