Na. Charles Kusaga, Kibaha - PWANI
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeendesha semina ya elimu kuhusu mabadiliko ya sheria za kodi kwa mwaka 2026, iliyowakutanisha wafanyabiashara, wahasibu, watoa huduma za kodi na wadau mbalimbali katika Ukumbi wa Destiny, Kibaha Mkoa wa PWANI
Lengo la semina hiyo lilikuwa kuwajengea walipakodi uelewa wa mabadiliko ya sheria za kodi, taratibu za ulipaji kodi pamoja na umuhimu wa kuzingatia sheria za kodi ili kuongeza uwajibikaji na kuchangia maendeleo ya taifa.
Washiriki walipata fursa ya kuuliza maswali na kupata ufafanuzi kuhusu changamoto mbalimbali zinazowakabili walipakodi, huku wakihimizwa kuendelea kufuata sheria na kutumia huduma za kidijitali zinazotolewa na mamlaka hiyo.
TRA imeendelea kusisitiza kuwa elimu ya mlipakodi ni nyenzo muhimu katika kuongeza uelewa wa wananchi, kuboresha hiari ya ulipaji kodi na kuimarisha ushirikiano kati ya mamlaka na walipakodi.
Club News Editor
Comments
Post a Comment