RAIS SAMIA ATANGAZA KIBAHA MJINI KUWA MANISAPAA,MBUNGE KOKA AFURAHIA ASEMA KIBAHA ITANG'AA


Na Gustaphu Haule,Pwani

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ameridhia Halmashauri ya Mji Kibaha iliyopo Mkoani Pwani kupandishwa hadi na kuwa Manispaa.

Uamuzi huo umetangazwa leo Januari 27 na Waziri wa Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mohamed Mchengerwa Mjini Kibaha.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Mohamed Mchengerwa akizungumza katika mkutano wa CCM uliofanyika Januari 27 katika viwanja vya stendi ya zamani Mailimoja Kibaha Mkoani Pwani.

Mchengerwa, ametangaza hilo wakati akizungumza na wanachama wa CCM pamoja na Wananchi katika mkutano mkubwa wa kuunga mkono maazimio ya mkutano Mkuu wa CCM Taifa uliomteua Rais Samia kuwa mgombea wa Urais mwaka 2025.

Wanachama wa CCM pamoja na Wananchi mbalimbali walioshiriki mkutano wa kuunga mkono azimio la Mkutano Mkuu wa Taifa CCM la kumteua Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea pekee wa Urais kupitia CCM katika uchaguzi wa mwaka 2025, Mkutano huo umefanyika Januari 27 mwaka huu stendi ya zamani Mailimoja Kibaha Mkoani Pwani.

Mbali na Rais Samia lakini pia mkutano Mkuu wa CCM Taifa ulimteua Balozi  Emmanuel Nchimbi kuwa mgombea Mwenza huku upande wa Zanzibar ukimteua Dkt . Hussein Mwinyi kuwa Mgombea Urais Zanzibar mwaka 2025..

Mchengerwa, amesema kuwa Rais Samia anafanyakazi kubwa na haijawai kutokea na katika muda wake mfupi amepandisha hadhi Rufiji kuwa Mji na Halmashauri ya Mji Kibaha kuwa Manispaa.

Amesema, Kibaha Mjini imepiga hatua kubwa kimaendeleo na Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka amefanyakazi kubwa sana kwakuwa Mji sasa umebadilika.

Kutokana na mabadiliko makubwa ya kimaendeleo Mbunge Koka aliwasilisha ombi la kutaka Kibaha Mjini kuwa Manispaa na kwakuwa Kibaha Mjini inakwenda kasi kimaendeleo Rais Samia ameridhia Kibaha Mjini kuwa Manispaa.

"Leo hii Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka, amesema Kibaha imepiga hatua kubwa ya kimaendeleo na aliwasilisha ombi la kuwa Manispaa na Rais Dkt.Samia amekubali ombi hilo na Leo hii Kibaha Mjini imekuwa Manispaa,"amesema Mchengerwa.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka, amesema kuwa mkutano huo licha ya kuunga mkono azimio la mkutano Mkuu lakini imekuwa ni faraja kwa Wananchi wa Kibaha Mjini kupata Manispaa.

Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka, akizungumza katika mkutano wa kuunga mkono azimio la Mkutano Mkuu wa CCM Taifa uliomteua Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea pekee wa Urais kupitia CCM mwaka huu.

Koka, amesema kuwa Kibaha Mjini ndio Makao Makuu ya Mkoa wa Pwani na muda wote huo ilikuwa bado Halmashauri ya Mji lakini leo imekuwa furaha kubwa kwake kupata Manispaa.

Koka, amesema kuwa takribani miaka miwili amekuwa akiipigania Kibaha Mjini ili hiwe Manispaa ambapo katika kipindi hicho aliweza kupeleka maswali zaidi ya manne na amekuwa akifuatilia jambo hilo katika vikao mbalimbali kwa umakini na Serikali ikiwa inajibu kuwa inalifanyiakazi.

"Leo nafurahi kusema kwamba,katika mkutano huu wa kupitisha azimio la kumteua Rais Samia kuwa mgombea pekee wa Urais kupitia CCM,Waziri wa Tamisemi ametamka wazi kuwa Kibaha Mjini ni Manispaa,",amesema Koka

Koka, amesema kuwa Manispaa maana yake Kibaha imepanda kwakuwa kila kitu ambacho kitakuwa kinafanyika ikiwemo bajeti ,maslahi ya watumishi, yatapanda lakini hata bajeti ya kuhudumia Wananchi na yenyewe itaongezeka.

Koka, ameongeza kuwa kwasasa atahakikisha anakwenda kusimamia utaratibu wote wakimanispaa unaotakiwa ikiwemo kuendelea kuubadilisha Mji kuwa wakisasa kama ambavyo wameshapanga ili hiwe mfano wa kuigwa kwa Miji mingine.

"Leo siku ya furaha na tunaipongeza sana Serikali yetu chini ya Rais Dkt.Samia kwa uamuzi uliofikia baada ya maombi yetu ya muda mrefu kuhakikisha Kibaha Mjini inakuwa Manispaa,"ameongeza Koka

Aidha, Koka amesema kwa kipindi ambacho Rais Samia ameingia madarakani ameona maajabu makubwa ambayo hayakuwai kutokea katika Jimbo la Kibaha Mjini kwakuwa maendeleo yaliyopatikana ni makubwa.

Amesema,tangu aingie madarakani kushika nafasi ya ubunge mwaka 2010 barabara ya lami ilikuwa ni moja ambayo inatoka Tamko-Tumbi - Picha ya Ndege lakini leo sehemu kubwa Kibaha inalami.

Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM)  na Serikali wakiwa katika mkutano maalum wa kuunga mkono azimio la mkutano Mkuu wa CCM Taifa uliomteua Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea pekee wa Urais kupitia CCM katika uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika mwaka huu, mkutano huo umefanyika Januari 27 katika viwanja vya stendi ya zamani Mailimoja Kibaha Mkoani Pwani.

Koka,amesema kuwa mwaka huu  Kata zote za Kibaha zinakwenda kupata barabara za lami kupitia mradi wa Tacts ambapo mpaka sasa jumla ya Kilomita 21 zinakwenda kufanyiwa kazi na hivyo kufanya Kibaha Mjini kupiga hatua zaidi ya kimaendeleo.

Amesema kuwa, katika kipindi chote hicho Kibaha Mjini imepiga hatua kubwa ya kimaendeleo kwani mbali na barabara lakini kwa upande wa umeme na Maji kila mahali huduma hiyo imefika isipokuwa katika eneo la Pangani ambalo linachangamoto ya Maji licha ya kuwa upo mradi unatekelezwa na muda si mrefu Pangani itakuwa na Maji ya kutosha.

Mwisho.
Club News Editor

Comments

Popular posts from this blog

RC PWANI AONGOZA WAKAZI PWANI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA

BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJINI LAMPONGEZA MKURUGENZI WAKE KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA SAMBAMBA NA KUONGEZA MAPATO.