DK.NCHIMBI ATETA NA VYAMA VYA SIASA VYA UKOMBOZI
- Asema CCM itashinda kwa kishindo uchaguzi Serikali za Mitaa 2024 na uchaguzi Mkuu 2025
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Dkt. Emmanuel Nchimbi akizungumza wakati wa kufungua kikao cha kazi cha Makatibu Wakuu wa Vyama Sita rafiki vya Ukombozi Kusini mwa Afrika. Makatibu Wakuu hao ambao wamekutana Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere (MJNLS), iliyopo Kibaha, mkoani Pwani, leo Alhamis Januari 25, 2024, kujadili masuala mbalimbali, ni kutoka vyama vya SWAPO (Namibia), ZANU-PF (Zimbabwe), ANC (Afrika Kusini), MPLA (Angola) na FRELIMO (Msumbiji).
Mwandishi wetu Kibaha.
Katibu mkuu wa chama cha Mapinduzi Taifa Balozi Dkt. Emanuel Nchimbi amewahakikishia Makatibu Wakuu wa Vyama Sita vya Ukombozi wa Nchi za Kusini mwa Afrika kwamba chama cha Mapinduzi kina uhakika wa kushinda kwa kishindo katika changuzi za mwaka huu na mwaka kesho, kwa maana ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu mwaka 2025.
Dkt. Nchimbi ametoa kauli hiyo wakati akifungua kikao cha Makatibu Wakuu wa Vyama Sita vya Ukombozi wa Nchi za Kusini mwa Afrika kilichofanyika katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, iliyopo Kibaha mkoani Pwani.
Makatibu Wakuu wa Vyama Sita Marafiki vya Ukombozi Kusini mwa Kusini, wakiwa katika picha ya pamoja, wakati walipokutana kwa ajili ya kikao cha kazi kujadili agenda mbalimbali katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere (MJNLS) iliyopo Kibaha mkoani Pwani.Kauli hiyo aliitoa baada ya kuwapongeza Chama Cha ZANU - PF cha Zimbabwe kwa kuibuka na ushindi katika uchaguzi wao walioufanya .
Pia katibu Mkuu Dk Ncimbi amevitakia heri ya ushindi NAMIBIA NA AFRIKA KUSINI kwenye uchaguzi wao mkuu ambao wao wanaufanya baadae mwaka huu na ANC cha Afrika kusini ambacho kimesheherekea kumbukumbu ya miaka 112 tangu kuanzishwa kwake.
Wakuu wa vyama sita rafiki vya Ukombozi Kusini mwa Afrika, ambao wanakutana katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere (MJLNS), Kibaha, mkoani Pwani ni pamoja na Sophia Shaningwa, Katibu Mkuu wa chama cha SWAPO cha Namibia, Obert Moses Mpofu, Katibu Mkuu wa Chama cha ZANU- PF cha Zimbabwe, Fikile Mbalula, Katibu Mkuu wa Chama cha ANC cha Afrika Kusini, Francisco Mucanheia ambaye ni mwakilishi wa Katibu Mkuu wa chama cha FRELIMO cha Msumbiji,Manuel Domingos Augusto na mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Chama cha MPLA nchini Angola .
Comments
Post a Comment