RAS PWANI KUANZA ZIARA MANISPAA YA KIBAHA AMSIFU DKT .ROGER'S SHEMWELEKWA KWA UKUSANYAJI MAPATO



Na Gustaphu Haule,Pwani 

KATIBU Tawala wa Mkoa wa Pwani Pili Mnyema, ameanza ziara yake ya kikazi katika Halmashauri za Mkoa wa Pwani kwa kutembelea Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha.


Katika ziara hiyo, Mnyema amesisitiza umuhimu wa ubunifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ili kuongeza mapato ya Halmashauri pamoja na Mkoa kwa ujumla.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Pili Mnyema katika kikao na watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha alipofanya ziara ya kuzungumza na watumishi wa Manispaa hiyo Agosti 12, 2025


"Naomba tumuunge mkono mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kubuni vyanzo vipya vya mapato na hii ni miongoni mwa maagizo niliyopatiwa ili kusaidia kuongeza mapato ya Mkoa wetu," amesema  Mnyema.

Aidha, amempongeza Mkurugenzi wa Manispaa ya Kibaha Dkt.Rogers Shemwelekwa kwa kuendelea kubuni na kusimamia miradi mbalimbali yenye tija, ambayo imesababisha ongezeko la mapato ya Manispaa hiyo kila mwaka.

Mnyema, amewataka watumishi wa Manispaa hiyo kuendelea kufanya kazi kwa kuzingatia misingi ya utumishi wa umma kwa kuwa na nidhamu, uadilifu, na bidii, ili kutoa huduma bora kwa wananchi. 

Watumishi wa Manispaa ya Kibaha wakimsikiliza kwa makini Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Pili Mnyema katika kikao kilichofanyika Agosti 12 , 2025 .


Amesisitiza pia umuhimu wa uwajibikaji na uaminifu katika usimamizi wa fedha za umma ili kudhibiti upotevu wa rasilimali na kuongeza ufanisi katika miradi ya maendeleo.

Akiwa katika Manispaa ya Kibaha, Katibu Tawala huyo ametembelea na kukagua miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa Shule ya Awali na Msingi ya mchepuo wa Kiingereza Mwalimu Nyerere iliyopo Kata ya Sofu, pamoja na mradi wa maduka ya biashara ya Kibaha Shopping Mall.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Kibaha Dkt.Rogers Shemwelekwa akieleza jambo kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Pili Mnyema (Kushoto)alipofanya ziara leo kwa ajili ya kukagua miradi ya maendeleo ya Manispaa ya Kibaha.

Ziara hiyo inalenga kukagua miradi ya maendeleo pamoja na kufanya vikao kazi na watumishi wa Halmashauri zote za Mkoa wa Pwani ambapo hatahivyo  Katibu Tawala anatarajiwa kuendelea na ziara hiyo kwa kutembelea Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe.

Club News Editor

Comments

Popular posts from this blog

RC PWANI AONGOZA WAKAZI PWANI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA

BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJINI LAMPONGEZA MKURUGENZI WAKE KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA SAMBAMBA NA KUONGEZA MAPATO.

RAIS SAMIA ATANGAZA KIBAHA MJINI KUWA MANISAPAA,MBUNGE KOKA AFURAHIA ASEMA KIBAHA ITANG'AA