AWESO AKEMEA MATUMIZI MABAYA FEDHA ZA MAJI
- Aonya, vipo vya kuchezea ukishiba chezea kidefu au kitambi chako sio fedha za miradi ya maji
Waziri wa Maji Juma Aweso amezindua skimu ya maji inayohudumia zaidi wananchi 8,000 katika kata ya Chumbi Wilayani Rufiji na kuielekeza jumuia ya watumiaji huduma hiyo kuhakikisha pesa walizokubaliana zinakusanywa na kupelekwa benki kwenye akaunti .
Aweso ametoa maelekezo hayo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Chumbi Rufiji Mkoani Pwani na kusisitiza kuwa vipo vya kuchezea na sio pesa za miradi ya maji
‘’ Tunajua mmeweka pesa ambayo mmekubaliana unapotaka kuchota maji lazima uchangie ,niwasihi jumuia iayosimamia hili fedha inapokusanywa ipelekwe benki kwenye akaunti na nataka niwaambie vipo vya kuchezea ukishiba chezea kidefu chako au kitambi chako sio fedha za miradi ya maji tutashughulikiana’’ amesema na kuongeza
‘’Watu wametesema kwa
muda mrefu sana wakitafuta hii huduma ya maji ambayo leo hii imepatikana hapa Chumbi kwa iyo tunapojenga mradi wa maji
maana yake lazima wananchi wafurahie
matunda na kazi nzuri inayofanywa na Mbunge, Rais, madiwani na wenyeviti hivyo
niwasihi sana kuulinda na kuutunza kwa faida ya vizazi vya sasa na vijavyo’’
ameongeza
Akijibu ombi maalumu lililotolewa na Kaimu mkuu wa Wilaya ya Rufiji ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Mkuranga Hadija Nasri ya uhitaji ya huduma ya maji katika kitongoji cha Nyakipande Aweso amemuagiza Meneja wa wakala wa maji safi na mazingira vijijini (RUWASA ) Pwani Beatrice Kasimbazi kuhakisha wanapeleka huduma hiyo kwenye eneo hilo
Awali Mkuu wa Mkoa Abubakar Kunenge akitoa salamu amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya kwani mradi huu ni matokeo ya jitihada zake.
“’ Maji ni uhai na pia maji ni ibada huu mradi ni kielelezo cha miradi mingi
inayotelezwa na Rais katika Mkoa wa Pwani na Nchi nzima kwa hiyo
niamshukuru sana kwa niaba ya watu wa Rufiji na Pwani kiujumla”’ amesema
Kunenge
Naye Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi (CCM ) Wilaya Rufiji Kaswakala Mbonde amesema kuwa wao chama wanafuraha kuwa utekeleaji skimu hiyo ni utekelezaji Ilani ya uchaguzi ya chama hicho Ibara ya 97 na kuwapongeza wananchi waliopisha chanzo cha maji ili mradi huo utekelezeke.
Baadhi ya wananchi wa Chumbi wamesema wamefarijika kupata huduma hiyo
kwa sababu awali walikua wanatembea umbali mrefu wa zaidi ya kilomita nne
kufaya maji kwenye mabwaya ambayo hata hivyo hayakua salama kwa afya zao
Aidha mwa mujibu wa taarifa ya RUWASA Rufiji ni kwamba ujenzi wa mradi huo wa maji umegharimu sh. 722.3 milioni fedha za mfuko wa maji ( NWF) chini ya usimamizi wa wakala wa maji safi na mazingira vijijini na kwamba umekwishaanza kutoa huduma kwa jamii katika vijiji vitatu vya Chumbi A,B na C
Taarifa hiyo imeeleza kuwa mradi huo uliibuliwa na wananchi wenyewe mwaka 2020 na kuanzishwa kwa lengo la kusogeza na kungezeka kiwango cha upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama na ya kutosheleza kwa jamii wa kata ya Chumbi hivyo kusaidia kupunguza magonjwa yanayosababishwa na ukosefu wa maji safi na salama
Lengo jingine ni
kuwapunguzia adha ya kufuata maji kwa
umbali mrefu na kusababisha kutumia muda mwingi kutafuta maji hali ambayo
inapelekea pia kushindwa kujishughulisha
na shughuli zinguine za kiuchumi.
Comments
Post a Comment