SERIKALI YATOA MATREKTA KWA WAKULIMA KIBAHA






Na Gustafu Haule,Pwani

MKUU wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge, amesema Mkoa  umeanza kutimiza adhma ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt.Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi inayoweza kuilisha dunia.

Kunenge, ameyasema hayo Januari 26/2024 wakati akikabidhi matrekta matatu kwa mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson John yaliyotolewa na serikali kwa ajili ya wakulima wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha wanaofanya kilimo cha pamoja.

Amesema,Mkoa umeweka utaratibu wa kuhakikisha mabadiliko ya haraka yanaonekana na kuunga adhma ya Rais ya kulisha nchi jirani na dunia ambapo ameonyesha nia ya dhati kwa kuweka mazingira mazuri ikiwa ni pamoja na kuweka wataalamu, vitendea kazi na vifaa vingine vya kilimo.

Aidha,Kunenge ameipongeza Wilaya ya Kibaha kwa kutenga eneo lenye ukubwa wa hekari 1,650 kwa ajili ya kilimo cha pamoja  cha mazao ya kilimo biashara na kuunganisha kilimo na viwanda kwa ajili ya kutoa ajira.

 "Kilimo kiungane na uchumi wa buluu kupitia uvuvi na mifugo ambapo milioni zaidi ya 500 zimetolewa kwa ajili ya ranchi ndogo na bado mambo mengine makubwa yanakuja kupitia Serikali ya mama Samia,"amesema Kunenge 

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson John, amesema wameanzisha kilimo cha pamoja ili kukabiliana na uharibifu wa mazingira kwa kuwaunganisha vijana kwenye kilimo badala ya kuchoma mkaa.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Erasto Makala ameishukuru Serikali kwa kuipatia Halmashauri Trekta hizo na amesema kuwa matrekta hayo yatachagiza wakulima kulima kwenye kilimo cha kibiashara.











Club News Editor Julieth Ngarabali

Comments

Popular posts from this blog

RC PWANI AONGOZA WAKAZI PWANI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA

BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJINI LAMPONGEZA MKURUGENZI WAKE KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA SAMBAMBA NA KUONGEZA MAPATO.

RAIS SAMIA ATANGAZA KIBAHA MJINI KUWA MANISAPAA,MBUNGE KOKA AFURAHIA ASEMA KIBAHA ITANG'AA