NOTI BANDIA ZA ZAIDI YA MIL.13 ZADAKWA PWANI
- Baadhi zilishaingia kwenye mzunguko wa matumizi Msata
Mwandishi wetu.
Pwani.WATU wanne wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Pwani kwa tuhuma za kukutwa na noti za pesa bandia za thamani ya zaidi ya sh. 13 milioni pamoja na mtambo wa kutengeneza pesa hizo.
Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani Pius Lutumo amesema kukamatwa kwa watu hao waliokutwa na pesa sh.1,550,000 milioni kulitokana na baadhi yao kutiliwa shaka baada ya kufanya malipo ya kukodisha chumba kwenye moja ya nyumba ya kulala wageni huko Masata Mkoani humo.
Amewataja watuhumiwa hao ni Mbaraka Fundi (48)Zena Naringa (42)wakazi wa Buza Jijini Daresalaam wengine ni Masumuko Kiyogoma (54) Mkazi wa Goba na Elius Wandiba (50) mkazi wa kimara Suka Jijini Dar esalaam.
''Kukamatwa kwa watuhumiwa hao kulitokana na taarifa za raia mwema aliyetilia mashaka noti ya sh.10,000 aliyopokea kama malipo ya huduma katika nyumba ya kulala wageni huko Msata na tulipata taarifa hiyo kisha kuwakamata na baada ya mahijiano tulifanikiwa kuwabaini washirika wenzao waishio huko Daresalaa"amesema Lutumo
Nakuongeza"Tulipopekua kwenye makazi yao tuliwakuta na pesa za noti bandia sh.12,000,000 na mashine ya kutengenezea pesa bandia pamoja na malighafi zake'amesema
Lutumo amewataka wakazi Mkoani humo kuchunguza kwa makini pesa wanazopokea kutoka kwa wateja wao kwaajili ya malipo mbalimbali na pindi wanapotilia mashaka wasisite kutoa taarifa kwa vyombo vya sheria ili hatua za uchunguzi zichukuliwe.
Baadhi ya wananchi Mjini Kibaha wamesema utambuzi wa noti bandia kwao ni changamoto kwa sababu sio rahisi kutambua machoni kwa haraka na hivyo wameomba Serikali kutoa elimu zaidi ili iwe rahisi kwao kutambua wanapokuta nazo kwenye maeneo ya biashara
Comments
Post a Comment