DK .TINDWA AMWAGA SIMU JANJA CCM MKURANGA

Mjumbe wa kamati ya Uchumi ya Jumuiya ya Wazazi Taifa ambaye ni mjumbe wa kamati ya Siasa ya Mkoa wa Pwani Dk. Chakou Tindwa(kushoto)akimkabidhi mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani Mwinshehe Mlao(Kulia) simu 26 zenye thamani ya Sh.milioni 6.5 Kwa ajili ya kusajilia wanachama kieletroniki. Na Gustafu Haule,Pwani MJUMBE wa Kamati ya Uchumi ya Jumuiya ya Wazazi Taifa Dk.Chakou Tindwa ameendelea na jitihada za kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi(CCM) ambapo kwa sasa ameipiga tafu CCM kwa kutoa simu janja 26 zenye thamani ya Sh.milioni 6.5 zitakazotumika kusajili wanachama waliopo Wilayani Mkuranga. Dk.Chakou ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Pwani mbali na kusaidia simu hizo lakini pia amekabidhi kadi za CCM 12,500 kwa ajili ya kuwagawia wanachama waliopo Wilayani humo. Hatua ya Dk Chakou kutoa simu na kadi hizo ni sehemu ya utekelezaji wa aadi zake alizozitoa kwa kamati ya Siasa ya Wilayani Mkuranga siku chache zilizopita. Akikabidhi simu na kadi hizo kwa...