HIKI NDICHO KILICHOMUUA EDWARD LOWASSA



                Edward Lowassa enzi za uhai wake

Makamu wa Rais  Dk. Philip Mpango atangaza  kifo chake kwa niaba ya Rais  Samia Suluhu Hassan 

·      Lowassa amefariki baada ya kuugua magonjwa ya kujikunja utumbo, matatizo ya mapafu na shinikizo la damu. 

 Na mwandishi wetu.

Makamu wa Rais wa Tanzania Dk. Philip Mpango  ametangaza kifo cha Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa aliyefariki leo saa nane mchana katika taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Dar esalam Februari 10 , 2024

Makamu wa Rais ametoa tarifa hiyo kwa niaba ya Rais  Samia Suluhu Hassan kupitia Televisheni ya shirika la utangazaji la Taifa (TBC) ambapo pia  ametangaza maradhi yaliyokua yanamsumbua na kumsababishia kifo.

Kupitia taarifa hiyo, amesema Lowassa amefariki baada ya kuugua magonjwa ya kujikunja utumbo , matatizo ya mapafu  pamoja na shinikizo la damu ,

Amebainisha kuwa hayati Edward Lowassa ameugua kwa muda mrefu na amekuwa akipatiwa matibabu tangu  Januari 14 ,2022 hospitalini hapo na baadae alipelekwa kwa matibabu zaidi nchini Afrika kusini ambapo alirejea tena JKCI alikopatwa na mauti leo hii.

“kutokana na kifo hicho Rais Samia ametoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki  na pia ametangaza siku tano za maombelezo ambapo bendera zitapepea nusu mlingoti kuanzia Februari 10 ,2024  na kwamba taarifa zaidi kuhusu msiba huu zitaendelea kutolewa na Serikali.

Hayati Edward  Lowassa amezaliwa Agosti 26,1953 katika kijiji cha Ngarash Monduli  na  kwamba katika familia ya mzee  Ngoyai Lowassa yeye ndiye alikua mtoto mkubwa wa kiume.



 

 



Club News Editor  Julieth Ngarabali

Comments

Popular posts from this blog

RC PWANI AONGOZA WAKAZI PWANI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA

BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJINI LAMPONGEZA MKURUGENZI WAKE KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA SAMBAMBA NA KUONGEZA MAPATO.

RAIS SAMIA ATANGAZA KIBAHA MJINI KUWA MANISAPAA,MBUNGE KOKA AFURAHIA ASEMA KIBAHA ITANG'AA