DK .TINDWA AMWAGA SIMU JANJA CCM MKURANGA
Mjumbe wa kamati ya Uchumi ya Jumuiya ya Wazazi Taifa ambaye ni mjumbe wa kamati ya Siasa ya Mkoa wa Pwani Dk. Chakou Tindwa(kushoto)akimkabidhi mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani Mwinshehe Mlao(Kulia) simu 26 zenye thamani ya Sh.milioni 6.5 Kwa ajili ya kusajilia wanachama kieletroniki.
Na Gustafu Haule,Pwani
MJUMBE wa Kamati ya Uchumi ya Jumuiya ya Wazazi Taifa Dk.Chakou Tindwa ameendelea na jitihada za kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi(CCM) ambapo kwa sasa ameipiga tafu CCM kwa kutoa simu janja 26 zenye thamani ya Sh.milioni 6.5 zitakazotumika kusajili wanachama waliopo Wilayani Mkuranga.
Dk.Chakou ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Pwani mbali na kusaidia simu hizo lakini pia amekabidhi kadi za CCM 12,500 kwa ajili ya kuwagawia wanachama waliopo Wilayani humo.
Hatua ya Dk Chakou kutoa simu na kadi hizo ni sehemu ya utekelezaji wa aadi zake alizozitoa kwa kamati ya Siasa ya Wilayani Mkuranga siku chache zilizopita.
Akikabidhi simu na kadi hizo kwa mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani Mwinshehe Mlao katika kikao cha kamati ya Siasa Wilayani Mkuranga kilichofanyika Februari 22 mwaka huu Tindwa amesema kazi ya kujenga chama ni jukumu la kila wanachama.
Mjumbe wa kamati ya Uchumi ya Jumuiya ya Wazazi Taifa na mjumbe wa kamati ya Siasa ya Mkoa wa Pwani Dk Chakou Tindwa (Kushoto) akimkabidhi mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani Mwinshehe Mlao(Kulia) kadi 12,500 kwa ajili ya kuwagawia wanachama wa CCM Wilayani Mkuranga.
Dk .Tindwa amesema simu hizo zitagawanywa katika kila Kata zilizopo Wilayani humo na kwamba dhamira yake ni kuona kila mwanachama anasajiliwa na kupata kadi ya kieletroniki kama ambavyo CCM Taifa ilivyoelekeza.
"Niliahidi kununua simu za kusajilia wanachama kwa njia ya kieletroniki hapa Wilayani kwetu Mkuranga na leo natimiza aadi yangu kwa kukabidhi simu hizi 26 zenye thamani ya Sh.milioni 6.5 naomba mwenyekiti uzipokee,"amesema Tindwa.
Aidha, Dk .Tindwa ameiambia kamati ya Siasa Wilayani Mkuranga kuwa yeye anamapenzi ya dhati na chama chake hivyo yupo tayari kuendelea kusaidiana na wanachama wenzake pamoja na wadau mbalimbali kuhakikisha wanakiimarisha chama kwa kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM) Mkoa wa Pwani Mwinshehe Mlao, akizungumza mara baada ya kupokea simu na kadi hizo amemshukuru Dk .Tindwa kwa namna anavyojitoa katika kuisaidia chama .
Mlao, amesema kuwa CCM haiwezi kujengwa na mtu mmoja bali itajengwa kwa ushirikiano wa wanachama, viongozi na wadau mbalimbali na kwamba kama kuna mtu anataka kuchangia chama ni vyema akajitokeza.
"Naomba nitumie fursa hii kumshukuru ndugu yetu Dk .Tindwa kwa msaada huu mkubwa kwani naamini kupitia simu hizi changamoto ya usajili kwa wanachama inakwenda kuisha,"amesema Mlao.
Hatahivyo, Mlao amewaomba Viongozi na wanachama ambao watakabidhiwa simu hizo kwenda kuzitumia kikamilifu kwa shughuli zilizokusudiwa ili kuweza kufikia malengo yaliyowekwa na chama.
Dk .Chakou Tindwa akizungumza katika kikao cha kamati ya Siasa cha Wilayani Mkuranga kilichofanyika Februari 22 mwaka huu.
ReplyForward |
Comments
Post a Comment