RATIBA RASMI MAZISHI YA HAYATI LOWASSA KUTOLEWA JUMANNE
Ratiba rasmi
ya mazishi ya Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa yanatarajiwa kutolewa Februari
13/2024 .
Kwa mujibu
wa taarifa iliyotolewa leo Februari 11 na
msemaji binafsi wa Lowassa , Aboubakar Liongo nyumbani kwa marehemu Masaki jijini Dar esalam ni kwamba ratiba hiyo itahusisha pia taratibu zote za
kiserikali.
“Taarifa
zaidi kuhusiana na tukio zima la mazishi zitatolewa baadae’’ amesema.
Hata hivyo
mwili wa Lowassa unatarajiwa kuzikwa
Februari 17/2024 katia kijiji cha Ngarash Wilayani Monduli mkoani Arusha .
Lowassa
amefarikia dunia Februari 10/2024 saa nane mchana jijini Dare salaam ambapo alikua
akipatiwa matibabu katika taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)
Taarifa za
kifo chake ilitolewa jana na makamu wa Rais, Dk. Philip Mpango.
Lowassa ambaye
hadi anafariki dunia alikua na umri wa miaka 70 alikua akipatiwa matibabu JKCI
ya magonjwa ya kujikunja utumbo,shinikizo la damu pamoja na matatizo ya mapafu.
“ Hayati Lowassa
alikua akipatiwa matibabu JKCI tangu tarehe 14/1/2022 na baadae alipelekwa
Afrika kusini kwa matibabu zaidi na baadae kurejea nchini “ amesema Dk. Mpango
alipokua akitangaza tukio la msiba huo.
Ameogeza kuwa akiwa nchini Afrika kusini , Lowassa alitembelewa na Waziri Mkuu Kassim Mjaliwa Desemba 28/2022 na kuwasilisha salamu za Rais, Samia Suluhu Hassan,
Comments
Post a Comment