DK, TINDWA AKUSANYA MIL 10.8 UJENZI OFISI YA CCM MKURAGA

- Ni katika harambee ya kuchangia ujenzi wa ofisi ya Kata CCM Shungubweni
Na Gustafu Haule,Pwani
MJUMBE wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Pwani Dr.Chakou Tindwa,ameendesha harambee ya kuchangia ujenzi wa ofisi ya CCM Kata ya Shungubweni iliyopo Wilayani Mkuranga na kufanikiwa kukusanya Sh.milioni 10.8.
Dr .Tindwa ameendesha harambee hiyo Februari 11 mwaka huu kwa kushirikiana na viongozi mbalimbali wa Halmashauri Kuu ya CCM Kata ya Shungubweni,huku ikihudhuriwa na viongozi wa Chama na Jumuiya kutoka Wilaya na Mkoa.
Kuwepo kwa Dr.Tindwa katika harambee hiyo kulitoa hamasa kwa WanaCCM na viongozi wengine kujitokeza na kumuunga mkono Dr.Tindwa ili kuhakikisha malengo ya ujenzi wa ofisi hiyo yanatimia
Dr.Tindwa mbali na kuendesha harambe hiyo lakini nae alichangia fedha taslimu Sh. milioni 5 na hivyo kuahidi kuendelea kushirikiana na WanaCCM wenzake kuhakikisha wanakijenga chama kwa pamoja.
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji kupitia Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Pwani Ahmed Salum (Kulia) akikabidhi Sh milioni mbili kwa Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Pwani Dr Chakou Tindwa (kushoto) kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya Kata Shungubweni Mkuranga
Dr Tindwa,amesema kuwa kiasi cha milioni 5 alichochangia ni mwanzo tu wa ujenzi wa ofisi hiyo lakini ataendelea kuchangia zaidi kadri mahitaji ya ujenzi wa ofisi hiyo yatakavyokuwa kwakuwa lengo ni kuhakikisha CCM inaendelea kuimarika.
"Nitaendelea kushirikiana na WanaCCM wenzangu katika kuhakikisha ofisi za CCM zinajengwa katika maeneo yote ambayo hayana ofisi na kufanikiwa kwa jambo hili ni ushirikiano tu,"amesema Dr.Tindwa.
Aidha,katika harambee hiyo Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji kupitia Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Pwani Ahmed Salum alimuunga mkono Dr .Tindwa kwa kuchangia fedha taslimu kiasi cha Sh.Milioni mbili.
Ahmed ,mara baada ya kuchangia fedha hizo amesema kuwa Chama Cha Mapinduzi(CCM) kitajengwa na wanachama wenyewe na kwamba wao kama viongozi wapo tayari kushirikiana na WanaCCM wenzao kuhakikisha chama kinakuwa na ofisi zao .
Hatahivyo,Ahmed amesema kuwa kuwepo kwa ofisi za chama katika Kata na hususani Kata ya Shungubweni kutaondoa changamoto ya kufanyia vikao chini ya miti ya Miembe.
Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Pwani Dr Chakou Tindwa akisalimiana na wanachama wa CCM kabla ya harambee ya ujenzi wa ofisi ya CCM Kata ya Shungubweni Wilayani Mkuranga .
Comments
Post a Comment