KIPANDE CHA VUMBI CHA BARABARA CHASABABISHA AJALI MSAFARA WA MAKONDA
- Magari zaidi ya 10 yagongana wakati msafara wa Makonda ukirejea Dar esalaam kujumuika na wananchi katika maombolezo ya kifo cha Lowassa
Zaidi ya magari 10 yaliyokua kwenye msafara wa
Katibu wa itikadi, uenezi na mafunzo wa chama cha Mapinduzi CCM Taifa , Paul
Makonda yamegongana leo katika kijiji cha Sululu Wilaya ya Masasi Mkoani
Mtwara.
Ajali hiyo
imetoka leo Februari 11 majira ya saa nane mchana katika eneo hilo wakati
msafara huo ukitokea Mkoani Ruvuma kuelekea Dar salaam.
Kwa mujibu
wa taarifa za awali kutoka kwa wakazi wa eneo hilo wamesema ajali hiyo imetokana na vumbi na
mwendo mkasi wa magari hayo ya msafara ambapo ilipofika kijijini hapo kwenye kipande
cha barabara ya vumbi moja ya gari ilipunguza mwendo kutokana na vumbi kubwa na
zito kwenye kipande cha barabara hali ambayo inaaminika ilisababisha mengine yaliyokua
nyuma kugongana na kuparamiana kwa nyuma.
“ mimi na
mdogo wangu tulikua tunasubiri kumuona Paul Makonda tumpungie mkono lakini
kutokana na vumbi la barabarani eneo tulipokuwa tulishindwa hivyo tukakaa
pembeni kabisa na ghafla baada ya magari kupita tukasikia kishindo cha magari
kugongana na baada ya dakika kadhaa tukabaini ni yale ya msafara”’ amesema
Bakari Musa
Kamanda wa
Polisi Mkoani humo Nicodemus Katembo
alipopigiwa simu amesema anafatilia tukio hilo na atatoa taarifa baadae.
Msafara huo
wa Makonda ulikua unarejea jijini Dar esalaam ukitokea Songea baada ya mapema
leo asubuhi kutangaza chama hicho
kusitisha ziara ya kiongozi huo katika mikoa ya Mtwara na Lindi iliyokua
imebaki katia ya 20 iliyolengwa na ziara hiyo.
Sababu kuu ya kusitishwa kwa ziara hiyo leo ni kutokana na kifo cha Waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa iliyotokea Februari 10 ambapo CCM inaungana na waTanzania katia maombolezo
Comments
Post a Comment