WAKILI MKOLWE-WANAFUNZI TOENI TAARIFA ZA UKATILI WA KINGONO ,ASEMA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA YA MAMA SAMIA IMEKUJA KUWAKOMBOA

Na Gustaphu Haule, Pwani MRATIBU wa Kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia ( Mama Samia Legal Aid Campaign) katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Vijijini Egidy Mkolwe, amewataka wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kilangalanga kuhakikisha wanatoa taarifa zinazoashiria ukatili wa Kingono. Mkolwe ambaye pia ni Wakili wa Serikali kutoka ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali ametoa wito huo wakati alipotembelea shuleni hapo akiambatana na timu ya wataalam mbalimbali katika utekelezaji wa kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia iliyoanza kufanyika leo Februari 25 katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Pwani. Mratibu wa Kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia katika Halmashauri ya Kibaha Vijijini Egidy Mkolwe alitoa elimu kuhusu masuala ya ukatili wa Kingono kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kilangalanga ikiwa ni sehemu ya kampeni hiyo iliyoanza Februari 25 mwaka huu Mkolwe, amewaambia wanafunzi hao kuwa zipo tabia na vitendo viovu vinavyoashiria ukatili wa Kingono ambavyo hu...