DOGO MABROUK AONGOZA SAMIA MARATHON KIBAHA VIJIJINI, ATOA UJUMBE KWA WANANCHI KUJITOKEZA KUPIGA KURA MWISHONI MWAKA HUU



Na Gustaphu Haule, Pwani 

MAKAMU mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Dogo Mabrouk ameongoza mbio za Samia Marathon iliyofanyika leo Februari 22,2025 katika viwanja vya Shule ya Msingi Mtongani Mlandizi Kibaha Vijijini.

Mabrouk, ameongoza mbio hizo akimwakilisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye ndiye alipaswa kuwa mgeni rasmi katika kuongoza mbio hizo.

Makamu mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Dogo Mabrouk akizungumza na Wananchi, viongozi wa chama na Serikali pamoja na WanaCCM kiujumla katika mkutano uliofanyika viwanja vya Shule ya Msingi Mtongani Mlandizi Kibaha Vijijini sehemu ambayo ilifanyika Samia Marathon chini ya maandalizi ya Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Pwani.

Mabrouk, katika mbio hizo aliongozana na viongozi wa chama na Serikali akiwemo Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Hamoud Jumaa ( MNEC) ambaye ni mkazi wa Mji wa Mlandizi, mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani,Mwishehe Mlao,Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge na Katibu Tawala MKoa wa Pwani Rashid Mchatta.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Hamoud Jumaa (MNEC)wa kwanza Kulia akiwa katika mbio za Samia Marathon zilizofanyika Februari 22 katika viwanja vya Shule ya Msingi Mtongani Mlandizi Kibaha Vijijini 

Akiwa katika, mbio hizo Mabrouk alikimbia umbali wa Kilomita tano ikiwa ni kutoka uwanjani hapo kupitia barabara ya ofisi ya CCM Mlandizi,Kituo cha Afya Mlandizi na kurudi uwanja ambapo akiwa uwanjani hapo alishuhudia mashindano mbalimbali yakiwemo ya kukuna nazi.

Akizungumza katika na Wananchi walioshiriki mbio hizo, Mabrouk amesema kuwa lengo la mbio za Samia Marathon ni kuhamasisha Wananchi kujitokeza kupiga kura katika uchaguzi mkuu ujao unaotarajia kufanyika mwishoni mwaka mwaka huu.

Mabrouk, amesema ameona watu wengi wamejitokeza katika kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura lakini mara nyingi kujitokeza kupiga kura wanakuwa wazito ndio maana watatumia mbio hizo kutoa elimu na kuhamasisha Wananchi kupiga kura.

"Nawaomba watu wote waliokuja hapa katika mbio hizo tujitahidi kuhakikisha tunajitokeza pia siku ya kupiga kura katika kuwachagua viongozi wetu akiwemo Rais, Wabunge na Madiwani,"amesema Mabrouk 

Aidha,katika hatua nyingine Mabrouk amesema kuwa Serikali ya awamu ya Sita inaongozwa na Mwanamke ambaye ni Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan amefanya mambo makubwa hivyo amewaomba Wananchi kumuunga mkono katika uchaguzi ujao.

Kwa upande wake Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Hamoud Jumaa,(MNEC) amesema kuwa mbio za Samia Marathon ni utekelezaji na makubaliano maalum ya viongozi wake wa juu katika kuhakikisha wanaendelea kuhamasisha Wananchi kutambua umuhimu wa kujitokeza katika kupiga kura ya kuwachagua viongozi wao.

Jumaa,amesema kuwa kufanyika kwa mbio za Samia Marathon katika Mji wa Mlandizi ni sehemu ya majaribio lakini wanategemea kufanya maandalizi ya mbio hizo kwa miaka mingine ya mbele katika Wilaya mbalimbali za Mkoa wa Pwani.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi MKoa wa Pwani Josian Kituka, ametumia nafasi hiyo kuwashukuru wadau mbalimbali waliofanikisha kufanyika kwa Samia Marathon huku akiomba na wengine wajitokeze zaidi katika kuendeleza mbio hizo.

Hatahivyo,Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge , ametumia nafasi ya mbio za Samia Marathon kueleza mafanikio ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Mkoa wake huku akisema suala la umeme Vijijini imefikia asilimia 98 huku maji yakifikia asilimia 83 na asilimia zilizobaki zitakamilika mwaka huu.

Mwisho 
Club News Editor

Comments

Popular posts from this blog

RC PWANI AONGOZA WAKAZI PWANI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA

BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJINI LAMPONGEZA MKURUGENZI WAKE KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA SAMBAMBA NA KUONGEZA MAPATO.

RAIS SAMIA ATANGAZA KIBAHA MJINI KUWA MANISAPAA,MBUNGE KOKA AFURAHIA ASEMA KIBAHA ITANG'AA