MBUNGE KOKA, AFUNGA MASHINDANO YA KIBAHA NDONDO CUP, AGAWA ZAWADI KEMKEM,AAHIDI KUONGEZA VIWANJA VYA KISASA.

 

Na Gustaphu Haule,Pwani

MBUNGE wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka, amefunga fainali za mashindano ya Kibaha Ndondo Cup yaliyokuwa yakifanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Mailimoja huku akiahidi kuendelea kuboresha michezo kwa kujenga viwanja vya kisasa.

Katika fainali hiyo iliyofanyika kati ya timu ya Sheli Fc kutoka Kata ya Mailimoja na timu ya Ungaunga Fc kutoka Kata ya Tangini iliwavutia Wananchi wengi lakini hata hivyo Ungaunga Fc aliibuka kuwa mshindi Kwa kupata bao 1-0.

Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka,akitoa zawadi ya Ng'ombe na Mpira Kwa mshindi wa mashindano ya Kibaha Ndondo Cup Ungaunga FC katika fainali  zilizofanyika  katika viwanja vya Shule ya Msingi Mailimoja, mashindano hayo yalikuwa chini CCM Kata ya Mailimoja 

Mashindano hayo ambayo yaliandaliwa na Chama Cha Mapinduzi ( CCM) Kata ya Mailimoja yamelenga kuibua vipaji lakini pia kuunga mkono jitihada za Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kuendeleza michezo hapa nchini.

Aidha, Koka ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mashindano hayo alikabidhi zawadi Kwa mshindi wa tatu aliyepata mipira miwili huku mshindi wa pili Sheli Fc akijinyakulia Mpira na  jezi  huku mshindi wa kwanza Ungaunga FC akiondoka na zawadi ya Ng'ombe pamoja na Mpira mmoja.

Akizungumza na Wananchi waliokusanyika katika fainali hizo Koka amesema anatambua changamoto ya uhaba wa viwanja vya  michezo na hata vile vilivyopo kuwa katika miundombinu mibovu .

Koka, amesema kwasasa ataanza kukarabati kiwanja cha mpira shuleni Mailimoja licha ya kuwa awali alitoa fedha za kutengeneza kiwanja hicho na sasa kinatumika vizuri lakini kinahitaji maboresho na ikiwezekana huko mbele kiwekwe nyasi bandia ili kiwe cha Kisasa zaidi.

Koka, ameongeza kuwa licha ya kiwanja hicho lakini pia Manispaa ya Kibaha inafanya utaratibu wa kuhakikisha kinapatikana kiwanja kingine upande wa Kata ya Pangani na kwamba baada ya miaka michache mbele Kibaha itakuwa na viwanja vya Mpira vya kutosha.

"Tunaona jinsi ambavyo Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan anavyowekeza katika michezo kwahiyo lazima nasisi tumuunge mkono ili kufikia malengo yake na mimi Mbunge wenu nitahakikisha Kibaha tunaboresha viwanja vilivyopo na ikiwezekana tupate viwanja vingine vipya ili kusudi Mpira Uchezwe,"amesema Koka.

Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka,akikabidhi zawadi ya jezi na Mpira kwa mshindi wa pili wa mashindano ya Kibaha Ndondo Cup ambayo ni timu ya Sheli Fc katika fainali zilizofanyika kwenye kiwanja cha Mailimoja Shuleni leo Februari 3,2025 , mashindano hayo yalikuwa chini ya Chama Cha Mapinduzi ( CCM) Kata ya Mailimoja 

Koka ,ameahidi kushirikiana na Wananchi pamoja na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kuhakikisha changamoto za miundombinu ya viwanja vya mpira zinafanyiwa kazi na hivyo kuwapa vijana fursa kuonyesha vipaji vyao.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Chama Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) Robert Munisi,amepongeza juhudi zinazofanywa na Mbunge huyo ikiwemo kukarabati uwanja wa Mailimoja Shuleni ambao hapo awali ulikuwa haufai kuchezewa mpira.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani Robert Munisi akizungumza katika fainali za Kibaha Ndondo Cup zilizofanyika katika kiwanja cha Shule ya Msingi Mailimoja kati ya timu ya Ungaunga FC ya Tangini na timu ya Sheli kutoka Kata ya Mailimoja.
"COREFA inamshukuru na kumpongeza Mbunge Koka kwa kazi kubwa anayoifanya kwani ameufanya uwanja huu kuwa mzuri na kuwezesha kuchezea Mpira lakini pia ametusaidia kupata eneo la ujenzi wa kiwanja huko Viziwa Viziwa hivyo lazima tumshukuru kwa kazi hiyo", amesema Munisi.

Mwisho 


Club News Editor

Comments

Popular posts from this blog

RC PWANI AONGOZA WAKAZI PWANI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA

BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJINI LAMPONGEZA MKURUGENZI WAKE KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA SAMBAMBA NA KUONGEZA MAPATO.

RAIS SAMIA ATANGAZA KIBAHA MJINI KUWA MANISAPAA,MBUNGE KOKA AFURAHIA ASEMA KIBAHA ITANG'AA