WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA KUONGOZA SAMIA MARATHON KIBAHA VIJIJINI, JACKSON KITUKA ASEMA NI MARATHON YA KIHISTORIA KUFANYIKA PWANI




Na Gustaphu Haule,Pwani

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa anatarajia kuwa mgeni rasmi katika kuongoza  mbio za polepole "Samia Marathon "zitakazofanyika Februari 22 mwaka huu Mlandizi Kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Pwani Josian Kituka, amewaambia Waandishi wa habari leo Februari 20 katika mkutano uliofanyika kwenye ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM )Mkoa wa Pwani zilizopo Kibaha Mjini.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani Josian Kituka akizungumza na Waandishi wa habari leo Februari 20 ofisini kwake kuhusu Samia Marathon inayotarajia kufanyika Februari 22 mwaka huu Mlandizi Kibaha Vijijini 

Kituka, amesema kuwa maandalizi ya mbio za Samia Marathon yamekamilika huku malengo yake ni kuhamasisha Wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa 2025.

Amesema kuwa, wameamua kutumia jina la Samia kwa ajili ya kumpa heshima Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ambaye amefanyakazi kubwa ya maendeleo katika kipindi kifupi alichokaa madarakani.
.


Kituka, amesema kuwa kutokana na hali hiyo Jumuiya wa wazazi Mkoa wa Pwani imeona ni vyema kuandaa marathon hiyo ilikusudi waongeze kasi ya kuhamasisha Wananchi kujitokeza kupiga kura katika uchaguzi mkuu ili kuhakikisha  Rais Samia anashinda kwa kishindo.

Amesema kuwa, Mbio hizo zitaanzia katika viwanja vya Shule ya Msingi Mtongani na kuelekea barabara ya Ruvu ikiwa ni umbali wa Kilomita tano,tatu na mbili ambapo Waziri Mkuu ataongoza mbio hizo kwa umbali wa kilomita tano.



"Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Pwani imeandaa mbio za Samia Marathon ambazo zinafanyika Kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani Februari 22 na tunatarajia kuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuwa mgeni rasmi" amesema Kituka

Aidha, Kituka amesema katika mbio hizo wanatarajia kuwa na washiriki 7000 kutoka ndani ya Mkoa na hata nje ya Mkoa huku akiwaomba Wananchi wajitokeze zaidi siku ya tukio hilo.

Amesema, kwakuwa jambo hilo limeandaliwa na Mkoa  kutakuwa na washiriki kutoka Wilaya zote za Mkoa wa Pwani huku akiendelea kuwaomba Wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki mbio hizo kwakuwa hakuna kiingilio.

Hatahivyo,Kituka amesema kuwa pamoja na mambo mengine lakini pia  Samia Marathon itapambwa na burudani mbalimbali wakiwemo wasanii wa Bongo Fleva,bendi za muziki ikiwemo Twanga na Kupepeta pamoja na vikundi vingine vya sanaa.

MWISHO 

Club News Editor

Comments

Popular posts from this blog

RC PWANI AONGOZA WAKAZI PWANI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA

BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJINI LAMPONGEZA MKURUGENZI WAKE KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA SAMBAMBA NA KUONGEZA MAPATO.

RAIS SAMIA ATANGAZA KIBAHA MJINI KUWA MANISAPAA,MBUNGE KOKA AFURAHIA ASEMA KIBAHA ITANG'AA