MNEC JUMAA AWAFUNDA MAKATIBU UENEZI KIBAHA MJINI, ATAKA WAENDE KUTANGAZA KAZI ZA RAIS SAMIA
Na Gustaphu Haule, Pwani
Makatibu Uenezi,Siasa na Mafunzo wa matawi na Kata wa Kibaha Mjini wakishiriki semina iliyofanyika katika viwanja vya Kibaha Shopping Mall Februari 11,2025 ,semina hiyo imeandaliwa na CCM Kibaha Mjini
Club News Editor
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi ( CCM) Hamoud Jumaa(MNEC) amefungua semina ya makatibu wa Itikadi, Uenezi, Siasa na Mafunzo wa Kibaha Mjini na kuwataka waende kufanyakazi ya kutangaza kazi zilizofanywa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Jumaa, amefungua mafunzo hayo Februari 11,2025 katika ukumbi wa Kibaha Shopping Mall uliopo karibu na stendi Kuu ya Mabasi ya Mkoani iliyopo Kibaha Mjini mafunzo ambayo yameandaliwa na CCM Kibaha Mjini.
Jumaa, amesema kuwa yapo mambo mengi CCM imetekeleza chini ya Dkt.Samia Suluhu Hassan hivyo lazima kazi hizo zielezwe kwa Wananchi pamoja na wanaCCM wote ambapo kwa kufanya hivyo watakuwa wamemtendea haki Rais Samia.

Amesema kuwa mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi mkuu na CCM inahitaji kuendelea kushika dola hivyo makatibu hao wanapaswa kufanyakazi kubwa ya kuhakikisha yale yote yaliyofanywa na Serikali ya awamu ya Sita chini ya Dkt .Samia yanawafikia Wananchi na wanaCCM wote.
"Natumia nafasi hii kuwaeleza kuwa huu ni mwaka wa uchaguzi hivyo nendeni mkiwa kitu kimoja na mkatumie mitandao ya kijamii kueleza mambo mazuri yaliyofanywa na Rais Dkt.Samia na CCM kwa ujumla ambapo kufanya hivyo tutakuwa tumemtendea haki Rais Samia na Chama chetu,"amesema Jumaa
Aidha, Jumaa amewataka viongozi hao kujiheshimu, kujitambua na kufanyakazi kwa maadili na muongozo wa chama na waache kununuliwa kirahisi na watu ambao wanajipitisha kwa kutaka kugombea nafasi za udiwani na ubunge ili hali wakati wa kufanya hivyo bado.
Aidha, katika mkutano huo Jumaa amempongeza Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka kwa kazi kubwa aliyoifanya katika Jimbo la Kibaha Mjini huku akiwaomba makatibu hao kuacha kuyumbishwa na mtu yeyote.
Jumaa, ameongeza kuwa Koka amefanyakazi kubwa ya kuleta maendeleo Kibaha Mjini ukilinganisha na wabunge wengine waliopita katika Jimbo hilo ambao amewaomba waendelee kutoa ushirikiano kwake ili Kibaha Mjini iweze kujengewa zaidi kimaendeleo.
"Nimpongeze Mbunge wa Kibaha Mjini Silvestry Koka kwa namna ambavyo amekuwa akipambana na maendeleo ya Jimbo hili, tumeshuhudia mambo mengi yamefanyika kupitia kwake na leo hii tumeona Kibaha Mjini imekuwa Manispaa kwahiyo tumpe ushirikiano ili aweze kufanya makubwa zaidi," amesema Jumaa
Jumaa, amesema Koka sio tu anafanyakazi za kusimamia miradi ya maendeleo lakini amekuwa mtu ambaye anafanyakazi za kukiimarisha chama chake kwa kufadhili mafunzo mbalimbali ya viongozi ikiwemo mafunzo na semina ya makatibu Uenezi yanayofanyika hivi sasa Kibaha Mjini.
Mwenyekiti wa CCM Kibaha Mjini Mwalimu Mwajuma Nyamka, amesema kuwa Kibaha Mjini ipo salama kwakuwa wanazingatia sera ya upendo,Umoja na mshikamano kwa kujua kuwa wote wanajenga nyumba Moja huku akiwataka makatibu hao kuwajibika katika maeneo yao.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kibaha Mjini Mwalimu Mwajuma Nyamka,katika semina ya makatibu Uenezi wa matawi na Kata wa Kibaha Mjini yaliyofanyika Februari 11,2025 katika eneo la Kibaha Shopping Mall lililopo karibu na stendi Kuu ya Mabasi ya Mjini Kibaha
Nyamka, amesema kuwa mwaka huu wanaelekea katika uchaguzi mkuu na walengwa wakubwa ni makatibu Uenezi na ili waweze kutambua umuhimu wa kipindi hiki lazima watambue majukumu yao.
Amesema, CCM Kibaha Mjini kwa kutambua umuhimu wa makatibu hao imeona ni vyema wakapewa mafunzo hayo ili kusudi wajengewe uelewa na hivyo waende kuwaeleza Wananchi na kufanya chama kiendelee kuimarika.
Kwa upande wake, Katibu wa Uenezi, Siasa na Mafunzo wa Kibaha Mjini Clement Kagaruki, amesema lengo la semina hiyo ni kuwajengea uwezo makatibu wake katika utendaji wa kazi zao za kila siku.
Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo wa CCM Kibaha Mjini Clement Kagaruki akizungumza katika semina ya makatibu Uenezi wa matawi na Kata iliyofanyika kwenye viwanja vya Kibaha Shopping Mall Februari 11,2025.
Kagaruki, amesema kuwa semina hiyo pia ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt.Samia Suluhu Hassan aliyetaka makatibu hao wajengewe uwezo wa kutekeleza Majukumu yao katika maeneo ya propaganda ,Chama na Serikali.
Kagaruki, amempongeza Mbunge wa Kibaha Mjini Silvestry Koka kwa ushauri na mawazo yake mazuri ya kuandaa semina hiyo ambayo kwa kiasi kikubwa inalenga kujiandaa na mapambano ya uchaguzi mkuu sambamba na kulipa deni kwa Rais Samia mwaka 2025 Kwa kumchagua kuwa Rais Kutokana na maendeleo makubwa aliyoyafanya.
Hatahivyo, Kagaruki amesema semina hiyo imehusisha makatibu Uenezi wa matawi na Kata kutoka Kibaha Mjini wapatao 95 huku ikihudhuriwa na wajumbe wa kamati ya Siasa akiwemo Mwenyekiti wa Vijana Kibaha Mjini Ramadhani Kazembe, Elizabeth Ngorika na Maguye.
Mwisho.
Comments
Post a Comment