IJUE SIRI YA JOSEPHINE MAENDAENDA KUCHAGULIWA MARA TATU KITONGOJI CHA JANGA.
Na Gustaphu Haule, Pwani UNAPOTAKA kuwataja wenyeviti wa Vitongoji Wanawake waliopo katika Halmashauri ya Kibaha Vijijini hutakosa kumtaja Josephine Maendaenda mwenyekiti wa Kitongoji cha Janga kilichopo Kata ya Janga. Maendaenda ameshinda katika uchaguzi wa Serikali ya Mitaa,Vijiji na Vitongoji uliofanyika Novemba 27 mwaka huu kwa kupata kura 2066 ushindi ambao unamfanya kuwa mwenyekiti wa Kitongoji cha Janga kwa awamu ya tatu mfululizo. Ushindi wa Maendaenda kwa Kitongoji hicho sio wa bahati mbaya bali nikusudio jema kwa Wananchi wake kutokana na umahiri wa kiuongozi katika vipindi viwili vya nyuma alivyowai kuongoza. Maendaenda ambaye pia ni mama mjasiriamali mwenye watoto wanne amekuwa na uzoefu mkubwa wa kiuongozi na hivyo kuwafanya Wananchi wake wafurahie kumchagua katika kila uchaguzi unapowadia. Maendaenda katika uchaguzi wake hakuwa na mpinzani ambapo wakati wa uchaguzi, mpiga kura alikuwa na chaguo la kutiki Ndio au Hapana jambo ambalo pia liliwapa wepe...