KAMPUNI YA DOWERCARE TECHNOLOGY YAGAWA TAULO ZA KIKE ZAIDI YA 20,000 KWA WANAFUNZI NCHINI



Na Gustaphu Haule,Pwani

KAMPUNI ya Dowercare Teknology ya Kibaha Mkoani Pwani imefanikiwa kuifikia jamii kwa kugawa bure taulo za kike  zaidi ya 20,000 kwa wanafunzi wa Shule mbalimbali hapa nchini.

Kampuni hiyo ambayo ni wazalishaji wa bidhaa mbalimbal ikiwemo pampanzi (pampers) vifutio vya watoto (Baby Wipes), Taulo za kike, sabuni za miche na zile za unga ikiwemo Doff ni miongoni mwa kampuni ambazo zimekuwa zikizalisha bidhaa zenye ubora hapa nchini.

Afisa Masoko wa kampuni hiyo Lucia Msami, amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maonesho ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji yanayofanyika katika viwanja vya stendi ya zamani Mailimoja Kibaha Mkoani Pwani.
Afisa Masoko wa kampuni ya Dowercare Technology Lucia Msami akiwa katika maonesho ya Viwanda Biashara na Uwekezaji katika viwanja vya stendi ya zamani Mailimoja Kibaha Pwani.

Amesema kuwa,kampuni yake imekuwa ikigusa jamii hususani watoto wa kike kwa kugawa taulo bure mashuleni na kwamba kwa mwaka 2023/2024 wamefanikiwa kuwagawa zaidi taulo zakike 20,000 kwa Shule mbalimbali hapa nchini.

Msami, amesema kuwa utaratibu huo pia  umefanyika kwa wanawake waliojifungua katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo wametoa taulo hizo bure kwa muda wa mwaka mmoja ambapo utaratibu huo unafanyika katika hospitali ya Teule ya Rufaa Tumbi iliyopo Mkoani Pwani na hospitali ya Temeke iliyopo Jijini Dar es Salaam.

 Msami ameishukuru Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa namna inavyotoa ushirikiano mzuri katika masuala ya Uzalishaji na Uwekezaji.

Akijibu ombi la Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega aliyepita katika Banda la kampuni hiyo wakati wa kufunga maonesho hayo tarehe 20 Disemba 2024 kuhusu suala la kupunguza bei za taulo za kike kwa wanafunzi waliopo shuleni. Msami amemuambia Waziri Ulega kuwa ombi la kupunguza gharama za taulo hizo tayari wameanza kulifanyia kazi ambapo kwa sasa wanafunzi wananunua taulo hizo kwa Sh.1200 huku Wanawake Vijijini wamekuwa wakinufaika kupitia Wakala waliopo katika maeneo hayo.

Afisa Masoko wa kampuni ya Dowercare Technology Lucia Msami (Kulia) akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega aliyetembelea banda la kampuni hiyo kabla ya kufunga maonesho ya Viwanda Biashara na Uwekezaji katika viwanja vya stendi ya zamani Mailimoja Kibaha Mkoani Pwani.

Hatahivyo, Msami amewaomba wananchi na Watanzania kwa ujumla kutumia bidhaa hizo kwakuwa zina gharama nafuu na  zimetengenezwa kwa ubora wa hali ya juu na hazina madhara kwa mtumiaji.

Afisa Masoko wa Kampuni ya Dowercare Technology ya Kibaha Mkoani Pwani Lucia Msami (katikati) akitoa elimu kwa Wananchi  juu ya bidhaa zinazozalishwa katika kiwanda hicho, kampuni hiyo ilikuwa katika maonesho ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji katika viwanja vya stendi ya zamani ya Mailimoja.

Akifunga maonesho hayo Waziri Ulega amesema Serikali itaendelea kushirikiana na wawekezaji hapa nchini kutatua vikwazo vinavyowakabili ikiwemo miundombinu ya barabara.

Mwisho.

Club News Editor

Comments

Popular posts from this blog

RC PWANI AONGOZA WAKAZI PWANI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA

BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJINI LAMPONGEZA MKURUGENZI WAKE KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA SAMBAMBA NA KUONGEZA MAPATO.

RAIS SAMIA ATANGAZA KIBAHA MJINI KUWA MANISAPAA,MBUNGE KOKA AFURAHIA ASEMA KIBAHA ITANG'AA