STAMICO YAWASHAURI WATANZANIA KUTUMIA NISHATI SAFI YA KUPIKIA , YASEMA INAOKOA GHARAMA


Na Gustaphu Haule,Pwani

SHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limewashauri Watanzania kutumia Nishati SAfi ya Kupikia  inayotengenezwa na Shirika hilo kwakuwa Nishati hiyo inasaidia kutunza mazingira pamoja na kuokoa gharama za maisha .

Afisa Masoko wa STAMICO  Hope Mahokola,ametoa ushauri Desemba 20 wakati akizungumza na waandishi habari katika maonesho ya Viwanda Biashara na Uwekezaji yanayofanyika katika viwanja vya stendi ya zamani Mailimoja Kibaha Mkoani Pwani.


Mahokola, amesema kuwa Nishati Safi  ya kupikia inayotengenezwa na Shirika hilo inatokana na mabaki ya  Makaa ya Mawe ambayo ni rafiki kwa mazingira hivyo ni vyema  jamii ikatumia Nishati hiyo.

Amesema kuwa,ajenda ya Nishati Safi ya kupikia ni ajenda ya Rais kwakuwa malengo yake ni kuifanya nchi hiwe salama katika kuondokana na adha ya uharibifu wa mazingira unaotokana na kukata kuni na mkaa.

Afisa Masoko wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Fatuma Msumi (kushoto)akitoa elimu ya matumizi ya Nishati Safi ya kupikia kwa Wananchi waliokuwa wakitembelea Banda la Shirika hilo katika maonesho ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji yaliyofanyika viwanja vya stendi ya zamani Mailimoja Kibaha Pwani.

Mahokola, ameongeza kuwa kwasasa Nishati hiyo inazalishwa  katika Viwanda vitatu vilivyopo nchini  kikiwemo kiwanda cha Trido kilichopo Msasani Jijini Dar es Salaam,Kiwanda cha Kisarawe katika eneo la Visegese, na Kiwanda cha Kiwila Mkoani Songwe.

Amesema kuwa, kwasasa STAMICO inampango wa kufungua kiwanda kingine katika eneo la Chigongwe Mkoani Dodoma pamoja na Mkoani Tabora ambapo lengo kubwa ni kuhakikisha Nishati Safi ya kupikia inapatikana nchini kote.

Mteja wa Nishati Safi ya kupikia inayotengenezwa na Shirika la Madini la Taifa STAMICO Avelin Laswai akikagua Nishati hiyo sambamba na kuonja nyama iliyochomwa kupitia Nishati hiyo katika banda la Shirika hilo lililokuwepo katika maonesho ya Viwanda Biashara na Uwekezaji Kibaha Mailimoja Mkoa wa Pwani.

"Nawashauri Watanzania wote kutumia Nishati Safi ya kupikia inayotengenezwa na STAMICO kwakuwa manufaa yake ni makubwa hasa katika kutunza mazingira na hata katika kuokoa gharama za maisha,"amesema Mahokola 

Mahokola, amesema Nishati hiyo inapatikana kwa bei rahisi kwani unaweza kununua Kilo 1 kwa gharama ya Sh  .1000 na unaweza kupikia zaidi ya masaa Nne jambo ambalo ni tofauti na mkaa wa Kuni ambao gharama yake kubwa na matumizi yake madogo.

Hatahivyo, amesema kwasasa Nishati hiyo inapatikana kirahisi katika ofisi za Upanga na Kwa Mawakala wa Jijini Dar es Salaam na Tanzania nzima kupitia vikundi vya akina mama (Wanawake na Samia)vya kila Mkoa ambapo Stamico ndio walezi wake.

Mwisho 


Club News Editor

Comments

Popular posts from this blog

RC PWANI AONGOZA WAKAZI PWANI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA

BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJINI LAMPONGEZA MKURUGENZI WAKE KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA SAMBAMBA NA KUONGEZA MAPATO.

RAIS SAMIA ATANGAZA KIBAHA MJINI KUWA MANISAPAA,MBUNGE KOKA AFURAHIA ASEMA KIBAHA ITANG'AA