Posts

Showing posts from October, 2023

WATU WATATU WAFARIKI AJALINI MKOANI PWANI

Image
  Na. Julieth Ngarabali,   Pwani.   Watu watatu wamepoteza maisha jana katika ajali ya barabarani ikihusisha magari mawili kugongana uso kwa uso huko Kijiji cha Mbala, Kata ya Vigwaza Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani majira ya saa 3 usiku Oktoba 23/2023   Kwa mujibu wa Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Pwani, Pius Lutumo ajali hiyo imehusisha gari dogo aina ya Kluger lenye namba T.478 DCQ ikitokea Iringa kwenda Dsm likiwa na watu 7 wa familia moja   aligongana na gari lenye namba T.851 AQC aina ya Scania.   Lutumo amesema katika ajali hiyo watu wanne walijeruhiwa ambao ni Amina Kondo miaka 77 na mtoto wa mwaka mmoja Abdallah Ally wote wakati wa Manzese Dar esalaam.   Majeruhi wengine wawili bado hawajafahamika majina yao kutokana na kutoweza kuzungumza,, wote walikimbizwa Hospitali ya Msoga Chalinze kwa matibabu   Majeruhi hao wanne pamoja na   watu watatu waliopoteza maisha wote walikua kwenye gari hilo dogo la Kluger ...

SERIKALI MKOANI PWANI YAANZA KUCHUKUA TAHADHARI MVUA ZA ELNINO, YAGAWA VIWANJA BURE KWA WANANCHI WAKE

Image
  Na Gustafu Haule, Pwani   SERIKALI Mkoani Pwani imeanza kuchukua hatua ya kufanya maandalizi juu ya kuwasaidia wananchi kuepukana na maafa yanayotokana na mvua   za Elmino kama ambavyo imetangazwa na mamlaka za Hali ya Hewa Nchini(TMA).   Mkuu wa Mkoa wa Pwani   Mh. Abubakari Kunenge, ameanza kuchukua hatua hiyo leo Oktoba 19 katika Wilaya ya Rufiji Kijiji cha Mohoro Kata ya Mohoro   akiwa na   na timu yake ya kamati ya ulinzi na usalama pamoja na watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji akiwemo Mkurugenzi Mtendaji Michael Gwimile.   Hatua ambayo tayari imechukuliwa ni pamoja na kuwahamisha wananchi wa Mohoro waliopo kandokando ya Bahari ya Hindi na kuwapelekea eneo mpya   lenye mazingira mazuri ya kuishi hata katika nyakati za mvua.     Akizungumza na wananchi wa Kijiji hicho Mh. Kunenge amesema kuwa Serikali imeona ianze kujipanga na kudhibiti maafa yanayotokana na mafuriko pindi mvua zinaponyesha kwa kuhakik...

TAIFA GAS YAONGOZA UZALISHAJI WA GESI NCHINI

Image
  Na Gustafu Haule, PWANI Kampuni ya   Taifa Gas inayoshughulika na   uingizaji na usambazaji   wa gesi imetajwa kuwa ni kampuni ya kwanza inayoongoza kwa uzalishaji wa gesi hapa nchini iliyofikia kiwango cha tani 7,440.   Mbali na kuongoza kwa uzalishaji lakini Taifa Gas ni kampuni iliyofanya uwekezaji mkubwa wa gesi   hapa nchini inayotokana na LPG (Liguidfield Petroleum Gas) ambayo haina madhara kwa mtumiaji. LPG ni bidhaa ya gesi inayotumika kama kimiminika cha Petroli kinachotokana na mafuta ghafi (Crude Oil) ambapo kupatikana kwake kunatokana na uyeyushaji katika joto kubwa.   Meneja Mkuu wa kituo cha kuhifadhia na usambazaji wa gesi ya Taifa Gas kilichopo     Kigamboni Jijini Dar es Salaam   Ndugu Juma Masese, amewaeleza waandishi wa habari kuwa   uzalishaji huo umepanda toka mwaka 2016 hadi sasa. Masese, amezungumza na waandishi wa habari wa mazingira na uhamasishaji jamii kutumia nishati mbadala waliofanya ziara ...

TANROAD PWANI YACHUKUA TAHADHARI KUKABILIANA NA MVUA ZA ELNINO

Image
  Na. Julieth Ngarabali . Pwani. Wakala wa barabara Mkoani Pwani  (TANROAD ) katika kukabiliana na mvua za Elnino zilizotabiriwa kunyesha Oktoba  imefanya matengenezo ya kinga katika barabara zake kuu zote,  kazi inayohusisha kufukua maeneo ya madaraja kwenye sehemu za kuingilia na kutokea maji na kufukua makalvati katika barabara ya Kibaha /Chalinze Morogoro, /Segera mpaka Manga na ya Kilwa road kwa maana ya Kongowe hadi Malendego.   Meneja wa TANROAD Pwani, Mhandisi Baraka Mwambage amesema kazi hiyo inafanyika baada ya kupata maelekezo ya Serikali kuhusu kuchukua tahadhari ya mvua za elnino .   Amesema walianza kwanza  kufanya ukaguzi wa madaraja yake yote 318 na makalvati 1,540  ya Mkoani wa Pwani kama hatua ya awali inayolenga kujua uharibifu na namna ya uhitaji wa matengenezo ulivyo na kisha ndio wakaingia kazini.   Mhandisi Baraka Mwambage ametoa  maekezo hayo  mara baada ya kutembelea na kukagua  maeneo hayo na kusisitiz...

HATUA ZA KINIDHAMU KUCHUKULIWA KWA VIONGOZI WALIOSHIRIKI UTAPELI KUUZA SHAMBA LA MIFUGO KWA WANANCHI

Image
  Na Julieth Mkireri,  KIBAHA PWANI MKUU wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Kibaha kuwachukulia hatua za kinidhamu viongozi walioshiriki kuwatapeli wananchi na kuuza maeneo katika shamba la mifugo Mitamba Kibaha.   Kunenge amesema wanaotakiwa kuchukuliwa hatua za kinidhamu ni pamoja na mabalozi kumi, watendaji wa Serikali wawili na wenyeviti wa Serikali za mitaa watano ambao wanatuhumiwa kushirikiana na matapeli kuwauzia ardhi wananchi kinyume cha sheria.   Ametoa maagizo hayo leo wakati akizungumza na wakazi wa Mtaa wa  Lumumba kata ya Pangani alipofanya mkutano kuzungumza na wananchi hao kuhusiana na maelekezo yaliyotolewa na serikali kwa wananchi waliovamia katika kiwanja namba 34.   Vile vile Kunenge amemuelekeza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani pamoja na Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Kuwafanyia mahojiano watuhumiwa 24 ambao wanatuhumiwa kuhusika na uuzaji wa ardhi katika shamba ...

UONGOZI MZURI NI ULE UNAOBADILISHA MAISHA YA WATU - Dkt BITEKO

Image
  Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati ,Mh. Dk.Doto Biteko Na. Julieth Ngarabali, Chalinze Pwani.   Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati ,Mh. Dk.Doto Biteko ametoa rai   kwa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM ) kufanya siasa za kubadilisha maisha ya wananchi katika kuwaletea maendeleo badala ya kufanya siasa za maneno matupu majukwaani na zisizojibu hoja.   Pia amewataka watumishi wa Umma kuwahudumia wananchi na kuwafuata walipo pasipo kuwasubiria walete kero zao kwenye madawati.   Ametoa rai hiyo   wakati akizungumza kwenye mkutano maalum wa jimbo la Chalinze wa kutoa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM kwa miaka miwili 2021/2022-2023 uliofanyika kwenye ukumbi wa shule ya Sekondari Lugoba.   Pichani Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati ,Dk.Doto Biteko (kulia) akiteta jambo na Mbunge wa Chalinze ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisini ya Rais Utumishi na utawala Bora,Ridhiwani Kikwete jana kwenye mkutano mkuu wa uwasil...

MISIME ATAKA WATU KUREJESHA SILAHA WANAZOMILIKI KINYUME NA SHERIA KWA SABABU HAWATAGUSWA NA MKONO WA DOLA.

Image
  Na. Julieth Ngarabali, Kibaha Pwani   Zoezi   la usalimishaji wa silaha mbalimbali za moto kwa hiyari linalofanyika nchi nzima limeonyesha kufanikiwa baada ya takwimu za silaha zinazosalimishwa maeneo mbalimbali kuongezeka kutoka silaha 228 mwaka 2021 ilipoanza utaratibu huo na kufikia 1,220 mwaka 2022 .   Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Kamishina Msaidizi Mwandamizi David Misime amesema hayo akiwa kwenye ziara ya kikazi Mkoani Pwani iliyolenga kutoa elimu kwa wananchi kuhusu usalimishaji wa silaha kwa hiyari zoezi linalofanyika nchi nzima.   Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Kamishina Msaidizi Mwandamizi David Misime (kushoto) akizungumza na vyombo vya habari mjini Kibaha leo,kulia ni kamanda wa Polisi Mkoani Pwani Pius Lutumo. Picha Julieth Ngarabali Amesema Mkoa wa Pwani ni miongoni mwa mikoa ambayo ilifanya vizuri kipindi hicho ambapo eneo hilo pekee ziliwasilishwa silaha 111 kati ya hizo.   Kamishina Msaidizi Mwandamizi Dav...

BODI YA MICHEZO YA KUBAHATISHA TANZANIA ( GBT) YAJENGA MRADI WA MAJI WENYE THAMANI ZAIDI YA MILIONI 64 SHULE YA SEKONDARI KIBAHA

Image
  Na Gustafu Haule, Pwani.   BODI ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT)imezindua na kukabidhi mradi wa maji katika Shule ya Sekondari Kibaha wenye thamani zaidi ya Sh.milioni 64 ikiwa ni sehemu ya kutatua changamoto ya ukosefu wa   maji katika Shule hiyo.   Mradi huo umezinduliwa leo Oktoba 12 na Mkurugenzi   Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania James Mbalwe ,hafla ambayo pia imeshuhudiwa na Mkurugenzi wa Shirika la Elimu Kibaha Robert Shilingi,walimu na wanafunzi.   Akizungumza mara baada ya uzinduzi huo Mbalwe,amesema kuwa bodi yake ilipokea ombi kutoka katika Shirika hilo kuhusu uhaba wa maji katika Shule ya Sekondari Kibaha na hivyo kulipa kipaumbele .   Amesema kuwa,baada ya kupokea maombi hayo Bodi iliona kuna umuhimu wa kusaidia Shule hiyo na hivyo kufanya jitihada za uchimbaji w na ujenzi wa tanki la ardhini la kuhifadhia maji lenye ujazo wa lita Laki moja pamoja na ununuzi wa matenki 10 yenye ujazo wa lita elfu ku...

WIZARA YA ELIMU,SAYANSI NA TEKNOLOJIA YAJA NA MPANGO MKAKATI WA MIAKA MITANO WA KUENDELEZA ELIMU YA WATU WAZIMA

Image
  Na Gustafu Haule,Pwani WIZARA ya Elimu ,Sayansi,na Teknolojia imeandaa Mpango Mkakati wa miaka mitano kuanzia mwaka 2020 hadi 2025 ambao umelenga kukuza na kuendeleza Kisoma na Elimu kwa umma (MTaKEU).   Mratibu wa kongamano la Kitaifa la maadhimisho ya Juma la Elimu ya watu Wazima Dkt.Sempeo Siafu,ametoa kauli hiyo leo Oktoba 12 wakati akifungua kongamano hilo lililofanyika Kibaha Mkoani Pwani.                                        Dkt.Siafu amesema kuwa mkakati huo uliandaliwa kwa makusudi kama nyenzo ya kuongoza wadau mbalimbali ambao wanatekeleza programu za kisomo na kwamba mpango huo unatambua kisomo kama haki ya msingi kwa maendeleo ya mtu binafsi, kijamii,kiuchumi na kisiasa. Aidha,amesema mbali na mpango huo lakini pia Wizara tayari imeandaa miongozo mitano ambayo inasaidia katika utekelezaji wa kuimarisha ubora wa utolewaji wa Elimu ya Sekondari kwa njia m...

TATIZO LA UMEME NCHINI KUISHA MIEZI SITA IJAYO, CHALINZE KUNUFAIKA UTEKELEZAJI ILANI YA UCHAGUZI (2020-2025)

Image
Na. Mwandishi Wetu, Pwani   Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mh. Dkt. Doto Biteko amesema katika kipindi cha miezi sita inayokuja ukosefu wa umeme nchini utaisha baada ya Serikali kuweka mikakati madhubuti ya kumaliza tatizo hilo nchini ambapo amesema Watendaji wanafanya kazi ili Watanzania wapate umeme wa kutosha. Ametoa ahadi hiyo katika Mkutano Mkuu Maalum wa Jimbo la Chalinze wa kupokea taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM (2020-2025) uliofanyika Wilaya ya Chalinze Shule ya Sekondari Lugoba .  Dkt. Biteko ameiagiza TANESCO  kuhakikisha inapeleka umeme katika Shule ya Sekondari ya Moreto ili Shule hiyo iunganishwe na umeme ,sambamba na hayo Dkt Biteko ameahidi kutoa kompyuta 10 kwenye Shule hiyo Ili ziwezs kuwasaidia Wanafunzi hao Katika Somo la TEHAMA. Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Mh. Ridhiwani Kikwete amesema, katika kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Rais Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze ime...

SHIUMA KIBAHA WAPEWA MREJESHO NAMNA YA KUNUFAIKA NA MIKOPO KUTOKA SERIKALINI

Image
Na. Mwandishi Wetu, Pwani Shirikisho la Umoja wa Machinga (SHIUMA) Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani wamemshukuru Mheshimiwa Rais Daktari SAMIA SULUHU HASSAN Kwa kuona umuhimu wa kuwatambua kama Kundi la wafanyabiashara nao kuweza kukopesheka na kupata fursa mbalimbali na kufikia malengo Katika Biashara zao.   Akizungumza katika Mkutano wa Shirikisho hilo wakati wa kutoa mrejesho kwa wafanyabiashara hao Mwenyekiti wa Machinga Mkoa wa Pwani Ndugu FILEMON MALIGA, alieleza namna ambavyo wametengewa maeneo na kuwezeshwa Shilingi Milioni kumi Kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya Shirikisho hilo na alieleza kuwa watakaa mahali pamoja na kuweza kukopesheka  Mwenyekiti wa Machinga Mkoa wa Pwani  Ndugu FILEMON MALIGA                                                   Katibu wa Mbunge Kibaha Mjini Ndugu Method Mselewa           ...