SHIUMA KIBAHA WAPEWA MREJESHO NAMNA YA KUNUFAIKA NA MIKOPO KUTOKA SERIKALINI
Shirikisho la Umoja wa
Machinga (SHIUMA) Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani wamemshukuru Mheshimiwa Rais Daktari
SAMIA SULUHU HASSAN Kwa kuona umuhimu wa kuwatambua kama Kundi la
wafanyabiashara nao kuweza kukopesheka na kupata fursa mbalimbali na kufikia
malengo Katika Biashara zao.
Wajumbe wa Mkutano wa Shirikisho la Umoja wa Machinga (SHIUMA) wakifuatilia Mkutano
Aidha Shirikisho hilo wakiwa wamemwalika Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Mh. Silvester Koka ambaye amewakilishwa na Katibu wake Ndugu Method Mselewa wamemuomba ushirikiano katika kuhakikisha wanafanikiwa kujenga Ofisi yao Ili waweze kukaa Mahali pamoja.
Akizungumza na wafanyabiashara hao Katibu huyo wa Mbunge Ndugu Mselewa amesema Serikali inawathamini sana wafanyabiashara hivyo nao wathamini mikopo wanayopewa na waweze kurudisha Kwa wakati sambamba na kuwahakikishia ushirikiano kutoka Ofisi ya Mbunge.
Aidha kwa upande wao
wafanyabiashara wamesema wanaishukuru Serikali kwa kutambua umuhimu wao kuwawezesha
na kuwajengea soko.
Comments
Post a Comment