WATU WATATU WAFARIKI AJALINI MKOANI PWANI

 


Na. Julieth Ngarabali,  Pwani.

 

Watu watatu wamepoteza maisha jana katika ajali ya barabarani ikihusisha magari mawili kugongana uso kwa uso huko Kijiji cha Mbala, Kata ya Vigwaza Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani majira ya saa 3 usiku Oktoba 23/2023

 

Kwa mujibu wa Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Pwani, Pius Lutumo ajali hiyo imehusisha gari dogo aina ya Kluger lenye namba T.478 DCQ ikitokea Iringa kwenda Dsm likiwa na watu 7 wa familia moja  aligongana na gari lenye namba T.851 AQC aina ya Scania.

 




Lutumo amesema katika ajali hiyo watu wanne walijeruhiwa ambao ni Amina Kondo miaka 77 na mtoto wa mwaka mmoja Abdallah Ally wote wakati wa Manzese Dar esalaam.

 

Majeruhi wengine wawili bado hawajafahamika majina yao kutokana na kutoweza kuzungumza,, wote walikimbizwa Hospitali ya Msoga Chalinze kwa matibabu

 

Majeruhi hao wanne pamoja na  watu watatu waliopoteza maisha wote walikua kwenye gari hilo dogo la Kluger

 

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Pwani Piusi Lutumo akizungumzia tukio la ajali iliyotokea usiku Oktoba 23 huko Mbala Mkoani Pwani na kusababisha vifo na majeruhi

Miili ya marehemu imehifadhiwa kituo cha afya Lugoba  Chalinze.

 

Mwisho.



Comments

Popular posts from this blog

MWENEZI CCM PWANI AKOLEZA MOTO USIKU WA COREFA,ASIFU MAANDALIZI YAKE

WIZARA YA AFYA YASEMA:UGONJWA WA SIKOSELI SIO WA KUROGWA, YAHAMASISHA JAMII KWENDA KUPIMA VINASABA

RAS PWANI KUANZA ZIARA MANISPAA YA KIBAHA AMSIFU DKT .ROGER'S SHEMWELEKWA KWA UKUSANYAJI MAPATO