UONGOZI MZURI NI ULE UNAOBADILISHA MAISHA YA WATU - Dkt BITEKO

 


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati ,Mh. Dk.Doto Biteko

Na. Julieth Ngarabali, Chalinze Pwani.

 

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati ,Mh. Dk.Doto Biteko ametoa rai  kwa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM ) kufanya siasa za kubadilisha maisha ya wananchi katika kuwaletea maendeleo badala ya kufanya siasa za maneno matupu majukwaani na zisizojibu hoja.

 

Pia amewataka watumishi wa Umma kuwahudumia wananchi na kuwafuata walipo pasipo kuwasubiria walete kero zao kwenye madawati.

 

Ametoa rai hiyo  wakati akizungumza kwenye mkutano maalum wa jimbo la Chalinze wa kutoa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM kwa miaka miwili 2021/2022-2023 uliofanyika kwenye ukumbi wa shule ya Sekondari Lugoba.

 

Pichani Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati ,Dk.Doto Biteko (kulia) akiteta jambo na Mbunge wa Chalinze ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisini ya Rais Utumishi na utawala Bora,Ridhiwani Kikwete jana kwenye mkutano mkuu wa uwasilishaji taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM kwa miaka miwili 2021/2022-2023 jimboni Chalinze uliofanyika kwenye ukumbi wa shule ya Sekondari Lugoba. Picha na Julieth Ngarabali

" ni wakati kwa wanaCCM kujibu kwa hoja kutokana na mafanikio makubwa yanayofanywa na Serikali kupitia ilani ya 2020-2025.,siasa za maneno mengi na matupu jukwaani zimepitwa na wakati, sasa tufanye siasa ya kubadilisha maisha ya wa Tanzania " amesema Dk. Biteko

 

Kuhusu taarifa ya utekelezaji wa Ilani iliyotolewa na Mbunge wa Chalinze ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisini ya Rais Utumishi, Mh. Ridhiwani Kikwete,  amesema  ameridhishwa na namna halmashauri ya Chalinze inavyosimamia fedha za miradi na ukusanyaji wa mapato.

 



"Nawapongeza kwa juhudi mnazofanya Chalinze  katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kijamii ikiwemo ujenzi wa madarasa, zahanati na miundombinu muhimu na pia kufanya vizuri katika makusanyo yenu mwaka ambapo mmeweza imekusanya shilingi 15  bilioni , kazi nzuri endeleeni kushikamana na mbunge wenu"amesema Naibu Waziri Mkuu huyo

 

Katika hatua ingine, , Dkt. Biteko ameiagiza TANESCO  kupeleka huduma ya umeme katika shule ya Sekondari ya Moreto  na pia ametoa kompyuta 10 kwenye shule hiyo kwa matumizi ya TEHAMA kuwasaidia wanafunzi kusoma vema masomoa yao ya sayansi

 

Akielezea utekelezaji wa ilani kwa miaka miwili iliyopita,Ridhiwani amesema utekelezaji umefikia asilimia 96 ,na sasa hatua waliyofikia inawabeba kutembea kifua mbele kwani huduma mbalimbali muhimu ikiwemo maji,umeme na vituo vya afya imewafikia wananchi


 Pichani Mh. Mbunge Ridwani  akielezea utekelezaji wa ilani kwa miaka miwili iliyopita


Ridhiwani ametolea mfano, sekta ya maji ,ameeleza awali ilipatikana kwa asilimia 62 kwa wananchi lakini sasa imefikia asilimia 96 ya upatikanaji maji jimboni humo

 

Ameongeza kuwa tayari sh. 6  Bilioni zimepokelewa katika Halmashauri ya Chalinze kutekeleza mambo mbalimbali ya maendeleo na kuondoa vikwazo vilivyokuwepo awali.

 


Rais Mstaafu  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete

Awali akitoa salamu kwa wajumbe wa mkutano huo, mgeni mualikwa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mkazi wa Chalinze Mh. Dkt.Jakaya Kikwete amesema, uteuuzi wa Naibu Waziri Mkuu Biteko sio jambo la kushangaza kwani ilishawahi kufanyika hilo la nchi kuwa na Naibu Waziri Mkuu ambapo kwa wakati huu Biteko anakua wa tatu.

 



Amesema ,Rais Samia Suluhu Hassan amefanya chaguo sahihi, katumia Mamlaka yake ya kikatiba na kwamba limekuja wakati sahihi na sio nafasi ya kubahatisha bahatisha hivyo ametaka Biteko achape kazi.


 

Mwisho


Comments

Popular posts from this blog

RC PWANI AONGOZA WAKAZI PWANI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA

BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJINI LAMPONGEZA MKURUGENZI WAKE KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA SAMBAMBA NA KUONGEZA MAPATO.

RAIS SAMIA ATANGAZA KIBAHA MJINI KUWA MANISAPAA,MBUNGE KOKA AFURAHIA ASEMA KIBAHA ITANG'AA