TATIZO LA UMEME NCHINI KUISHA MIEZI SITA IJAYO, CHALINZE KUNUFAIKA UTEKELEZAJI ILANI YA UCHAGUZI (2020-2025)
Dkt. Biteko ameiagiza TANESCO kuhakikisha inapeleka umeme katika Shule ya Sekondari ya Moreto ili Shule hiyo iunganishwe na umeme ,sambamba na hayo Dkt Biteko ameahidi kutoa kompyuta 10 kwenye Shule hiyo Ili ziwezs kuwasaidia Wanafunzi hao Katika Somo la TEHAMA.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Mh. Ridhiwani Kikwete amesema, katika kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Rais Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze imefanikiwa kutekeleza kwa kiwango kikubwa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020/25 ambapo amesema Katika hatua nyingine amewataka madiwani kuhakikisha wanashirikiana na Wananchi ili kutatua shida zao na kusukuma gurudumu la Chalinze .
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mh. Dkt. Doto Biteko amesema katika kipindi cha miezi sita inayokuja ukosefu wa umeme nchini utaisha baada ya Serikali kuweka mikakati madhubuti ya kumaliza tatizo hilo nchini ambapo amesema Watendaji wanafanya kazi ili Watanzania wapate umeme wa kutosha. Ametoa ahadi hiyo katika Mkutano Mkuu Maalum wa Jimbo la Chalinze wa kupokea taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM (2020-2025) uliofanyika Wilaya ya Chalinze Shule ya Sekondari Lugoba .
Dkt. Biteko ameiagiza TANESCO kuhakikisha inapeleka umeme katika Shule ya Sekondari ya Moreto ili Shule hiyo iunganishwe na umeme ,sambamba na hayo Dkt Biteko ameahidi kutoa kompyuta 10 kwenye Shule hiyo Ili ziwezs kuwasaidia Wanafunzi hao Katika Somo la TEHAMA.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Mh. Ridhiwani Kikwete amesema, katika kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Rais Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze imefanikiwa kutekeleza kwa kiwango kikubwa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020/25 ambapo amesema Katika hatua nyingine amewataka madiwani kuhakikisha wanashirikiana na Wananchi ili kutatua shida zao na kusukuma gurudumu la Chalinze .
Comments
Post a Comment