MISIME ATAKA WATU KUREJESHA SILAHA WANAZOMILIKI KINYUME NA SHERIA KWA SABABU HAWATAGUSWA NA MKONO WA DOLA.





 

Na. Julieth Ngarabali, Kibaha Pwani

 

Zoezi  la usalimishaji wa silaha mbalimbali za moto kwa hiyari linalofanyika nchi nzima limeonyesha kufanikiwa baada ya takwimu za silaha zinazosalimishwa maeneo mbalimbali kuongezeka kutoka silaha 228 mwaka 2021 ilipoanza utaratibu huo na kufikia 1,220 mwaka 2022 .

 

Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Kamishina Msaidizi Mwandamizi David Misime amesema hayo akiwa kwenye ziara ya kikazi Mkoani Pwani iliyolenga kutoa elimu kwa wananchi kuhusu usalimishaji wa silaha kwa hiyari zoezi linalofanyika nchi nzima.

 

Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Kamishina Msaidizi Mwandamizi David Misime (kushoto) akizungumza na vyombo vya habari mjini Kibaha leo,kulia ni kamanda wa Polisi Mkoani Pwani Pius Lutumo. Picha Julieth Ngarabali


Amesema Mkoa wa Pwani ni miongoni mwa mikoa ambayo ilifanya vizuri kipindi hicho ambapo eneo hilo pekee ziliwasilishwa silaha 111 kati ya hizo.

 

Kamishina Msaidizi Mwandamizi David Misime ameongeza sababu ya kuja Makao makuu ya Polisi  Pwani ni kuendeleza  kampeni hiyo ambayo Mkoa huo umeonyesha kufanikiwa na kutolea mfano katika kipindi hiki kifupi tu mwaka huu toka kampeni ianze septemba mosi tayari silaha 11 zimekwisha wasilishwa tangu zoezi hilo lilipoanza mwaka huu .

 

"Mwezi wa kampeni ya uwasilishaji silaha kwa hiari ambayo ilianza Septemba mosi na itamalizika Oktoba 31/2023 na kipindi hiki ndio kila mtu anayemiliki silaha kinyume na sheria anatakiwa kusalimisha kwa hiari na atakwepa kutokukamatwa,kutokufikishwa mahakamani na pia anakua huru kwa kuendelea na shughuli zake za kujiletea maendeleo "amesema  Misime.

 

Amewataka Polisi Kata kushirikiana na viongozi mbalimbali walioko kwenye maeneo yao katika kuhamasisha wananchi wanao miliki silaha kinyume cha sheria kusalimisha  silaha hizo kwa hiyari.

 

" Nasisitiza sana wananchi wanaoishi maeneo ya hifadhi (misitu) ya wanyama kuhakikisha wanarejesha silaha walizonazo ikiwemo ngorongoro, mikumi na, Serengeti

 

Zoezi la usalimishaji wa silaha litafika ukomo Oktoba 31 mwaka huu ambapo amelekeza Polisi Kata nchini kote kutumia muda mchache uliosalia kutoa elimu na kuwahamasisha wananchi wenye kumiliki silaha kinyume na sheria za nchi haswa wananchi wanao ishi maeneo yaliyo karibu na mbuga za wanyama.

 

Misime ameeleza kama kuna mtu ambaye anatambua ndani kwake kuna silaha ambayo ilikuwa ikimilikiwa na mtu ambaye alishafariki inapaswa kusalimishwa kabla ya tarehe 31 Oktoba na hawatachukuliwa hatua zozote za kisheria na kwa wale watakao kaidi baada ya hapo msako mkali utaanza na wale watakao kamatwa watachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kufikishwa Mahakamani.

 

"Nawapongeza Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani kwa kuwa miongoni mwa Mikoa inayofanya vizuri kwenye zoezi hili la usalimishaji wa silaha kwa hiyari na kutolea mfano Wilaya ya Kipolisi Chalinze ambapo idadi ya silaha 11 zimekwishasalimishwa tangu zoezi hilo lilipoanza mwezi huu uliopita" amesema Misime

 

Kadhalika, ametoa pongezi na kuwaomba viongozi wa Dini na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa na Vitongoji kuendelea kutoa ushirikiano katika zoezi hili la usalimishaji wa silaha na Jeshi la Polisi litaendelea kushirikiana nao ili kuhakikisha linapata mwitikio mkubwa kwa Jamii.

 

Awali Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani Pius Lutumo amesema hasara za kutosalimisha silaha katika kipindi hiki ni pamoja na itafanyika misako baada ya Oktoba 31 na hasara zake ni kukamatwa na kufikishwa mahakamani na ukipatikana na hatia kifungo chake ni miaka 15 au faini ya sh. 10 Milioni.

 

Mmoja wa wakazi wa Chalinze Seifu Ally amesema utaratibu huo ni mzuri na kuomba wengine kutii sheria bila shuruti.

Comments

Popular posts from this blog

RC PWANI AONGOZA WAKAZI PWANI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA

BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJINI LAMPONGEZA MKURUGENZI WAKE KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA SAMBAMBA NA KUONGEZA MAPATO.

RAIS SAMIA ATANGAZA KIBAHA MJINI KUWA MANISAPAA,MBUNGE KOKA AFURAHIA ASEMA KIBAHA ITANG'AA