MWENGE WA UHURU KUZINDUA MIRADI 126 YENYE THAMANI YA TRILIONI 8•5 PWANI

Na Gustafu Haule, Pwani MKUU wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge,amesema kuwa mbio za mwenge wa Uhuru zilizoanza leo Mkoani humu zinatarajia kufikia miradi 126 yenye thamani zaidi ya Trilioni 8.5. Kunenge,ametoa taarifa hiyo leo Aprili 29 wakati akipokea Mwenge huo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Adam Malima ambapo makabidhiano yake yalifanyika katika viwanja vya Jeshi la Magereza Bwawani katika Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze. Katika taarifa yake Kunenge amesema kuwa Mwenge wa Uhuru ukiwa Mkoani Pwani utapita katika Wilaya Saba na Halmashauri Tisa huku jumla ya miradi 126 itapitiwa ambapo kati ya hiyo miradi 18 itawekewa mawe ya msingi, miradi 22 itazinduliwa na miradi 86 itakaguliwa. Kunenge,amesema kuwa fedha za utekelezaji wa miradi hiyo imetoka sehemu mbalimbali ikiwemo Serikali Kuu, Halmashauri za Wilaya ,wadau na nguvu za Wananchi. Aidha , Kunenge ametumia nafasi hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ambaye ndi...