MWENGE WA UHURU KUZINDUA MIRADI 126 YENYE THAMANI YA TRILIONI 8•5 PWANI




Na Gustafu Haule, Pwani 

MKUU wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge,amesema kuwa mbio za mwenge wa Uhuru zilizoanza leo Mkoani humu zinatarajia kufikia  miradi 126 yenye thamani zaidi ya Trilioni 8.5.

Kunenge,ametoa taarifa hiyo leo Aprili 29 wakati akipokea Mwenge huo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa  Morogoro Adam Malima ambapo makabidhiano yake yalifanyika katika viwanja vya Jeshi la Magereza Bwawani katika Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze.



Katika taarifa yake Kunenge amesema kuwa Mwenge wa Uhuru ukiwa Mkoani Pwani utapita katika Wilaya Saba na Halmashauri Tisa  huku jumla ya miradi 126 itapitiwa ambapo kati ya hiyo miradi 18 itawekewa mawe ya msingi, miradi 22 itazinduliwa na miradi 86 itakaguliwa.

Kunenge,amesema kuwa fedha za utekelezaji wa miradi hiyo imetoka sehemu mbalimbali ikiwemo Serikali Kuu, Halmashauri za Wilaya ,wadau na nguvu za Wananchi.



Aidha , Kunenge ametumia nafasi hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ambaye ndiye aliyesaidia kuweka mazingira bora kwa ustawi na ufanisi katika kuleta maendeleo ya Taifa.

"Mwenge wa Uhuru mwaka huu utapitia miradi mikubwa na midogo 126 yenye thamani zaidi ya Trilioni 8.5 na katika miradi hiyo 18 itawekewa mawe ya msingi, 22 kuzinduliwa na 16 kukaguliwa kwahiyo tumejipanga vizuri kuhakikisha miradi yote inapitiwa kikamilifu," amesema Kunenge.

Kunenge,amesema kuwa kauli mbiu ya mwaka huu inaakisi maisha halisi ya Mtanzania kwani Mwenge huo umebeba ujumbe mahususi ambao unasema "Tunza Mazingira, Shiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa Kwa ujenzi wa Taifa endelevu".

Aidha, Kunenge amesema katika utunzaji mazingira Mkoa wa Pwani katika kipindi cha mwaka 2020/2024 ulikuwa na lengo la kupanda miche zaidi ya milioni 13•5 lakini mpaka kufikia Juni 2023 tayari miche milioni 8 ilikuwa imepandwa.

Hatahivyo, Kunenge amewahakikishia wakimbiza Mwenge kitaifa kuwapa ushirikiano mkubwa ili kuweza kutekeleza jukumu hilo muhimu Kwa maendeleo ya Taifa la Tanzania.



Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024 Godfrey Mnzava, amewataka Wataalamu wa idara mbalimbali Mkoa wa Pwani kutoa ushirikiano wa karibu pale ukaguzi wa miradi unapofanywa na wakimbiza Mwenge  ili kurahisisha utekelezaji wa jukumu hilo.


Club News Editor - Charles Kusaga







Comments

Popular posts from this blog

RC PWANI AONGOZA WAKAZI PWANI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA

BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJINI LAMPONGEZA MKURUGENZI WAKE KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA SAMBAMBA NA KUONGEZA MAPATO.

RAIS SAMIA ATANGAZA KIBAHA MJINI KUWA MANISAPAA,MBUNGE KOKA AFURAHIA ASEMA KIBAHA ITANG'AA