TFS WACHANGIA MILIONI 20 WAHANGA WA MAFURIKO KIBITI NA RUFIJI




Na Gustafu Haule,Pwani

WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) imetoa kiasi cha Sh.milioni 20 kwa ajili ya kusaidia kutatua Changamoto za wahanga wa mafuriko yaliyotokea katika Wilaya ya Kibiti na Rufiji  Mkoani Pwani.

Mfano wa hundi ya fedha hizo imekabidhiwa leo na meneja mahusiano wa TFS  nchini Johary Kachwamba kwa mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge katika hafla iliyofanyika ofisi za Mkuu huyo zilizopo Mjini Kibaha.

Kachwamba,amesema kuwa TFS kupitia Kamishna wake Silayo Dos Santos imeguswa na janga hilo la mafuriko ndio maana imeona kuna kila sababu ya kuunga mkono Serikali kwa kusaidia wahanga wa Wilaya hizo.




Amesema kuwa,TFS kwa eneo la Rufiji wanamisitu na kwamba wanaRufiji ni wahifadhi wenzao kwakuwa TFS ina misitu zaidi ya 10 ikiwa na zaidi ya hekta 32,000 ndio maana Kamishna wa Uhifadhi ametoa kiasi ili kusaidia wahanga hao.

Amesema,pamoja na kutoa mchango huo lakini bado TFS wataendelea kushika mkono katika kutatua changamoto mbalimbali pale ambapo itahitajika kwakuwa jambo hilo linahitaji ushirikiano wa pamoja.

"TFS kupitia Kamishna wa Uhifadhi Silayo Dos Santos ametoa kiasi cha Sh.milioni 20 kusaidia changamoto za wahanga wa mafuriko Rufiji na Kibiti lakini tutaendelea kushika mkono kulingana na mahitaji ," amesema Kachwamba.


Akizungumza mara baada ya kupokea hundi hiyo Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge,ameishukuru TFS kwa kwa mchango huo kwani wameonyesha namna ambavyo wameguswa na janga la mafuriko hayo.

Kunenge, amesema kuwa TFS wamefanya jambo hilo kwa ajili ya kumuunga mkono juhudi za Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan na kwamba kitendo hicho kinampa faraja Rais katika kuwatumikia Wananchi.



"Nawashukuru sana wenzetu wa TFS kwa kutoa mchango huu mkubwa kwa ajili ya kusaidia wahanga wa mafuriko Wilayani Kibiti na Rufiji,ni mfano wa kuigwa kwao kwakuwa wanaunga mkono Rais Samia,"amesema Kunenge 

Kunenge,amesema pamoja na kutoa mchango wa fedha hizo lakini TFS wameonyesha moyo wa pekee kwani kabla ya kutoa fedha hizo lakini tayari wametoa eneo na viwanja kwa ajili ya kufanyia shughuli za mafuriko.

Hatahivyo, Kunenge ameahidi kuzitumia fedha hizo katika kutoa huduma kwa wahanga wa mafuriko hayo huku akiwaomba TFS kuendelea kumuunga mkono Rais Samia na kuhakikisha wanatoka katika kutumia nishati ya mkaa na kwenda katika nishati mbadala.


Club News Editor -  Charles Kusaga



Comments

Popular posts from this blog

RC PWANI AONGOZA WAKAZI PWANI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA

BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJINI LAMPONGEZA MKURUGENZI WAKE KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA SAMBAMBA NA KUONGEZA MAPATO.

RAIS SAMIA ATANGAZA KIBAHA MJINI KUWA MANISAPAA,MBUNGE KOKA AFURAHIA ASEMA KIBAHA ITANG'AA