WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA ATAKA UMAKINI MATUMIZI YA TEKNOLOJIA
Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Dk Pindi Chana amewataka watumishi wa Wizara hiyo na Watanzania kwa ujumla kuwa makini na matumizi ya teknolojia hasa Ile ya akili bandia ili wasije wakapotoshwa katika kutoa au kupokea maamuzi mbalimbali ikiwemo za kesi zinazohitaji utafiti wa kutosha .
Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Dk Pindi Chana akifungua mkutano wa 20 wa Baraza la wafanyakazi wa tume ya kurekebisha sheria Tanzania
Balozi Chana amesema teknolojia ni nzuri lakini inahitajika umakini wa hali ya juu kwani kupitia baadhi ya mifumo maarufu ''Applications'' (Apps) inaweza ikatengeneza jambo au ikatoa hotuba fulani isio halisi na endapo hakutakuwepo umakini watu watafikiri kweli kumbe sio kweli.
Akili bandia "Artifial Intelligence" teknolojia iliyotengenezwa kwenye mifumo ya kompyuta kurahisisha kazi zinazotumia akili za kibinadamu
Waziri huyo amesema hayo akifungua mkutano wa 20 wa Baraza la wafanyakazi wa tume ya kurekebisha sheria Tanzania na.kwamba mkutano huo unafanyika kwa siku mbili kwenye ukumbi wa shule ya uongozi ya Mwalimu Nyerere Kwamfipa Kibaha Mkoani Pwani
Sehemu ya Washiriki wa mkutano wa 20 wa Baraza la wafanyakazi wa tume ya kurekebisha sheria Tanzania wakifuatilia jambo wakati wa mkutano huo.
"Hivi sasa unaposema Teknolojia kuja Apps za kila aina kiasi kwamba vitu vingi unaweza ukauliza kwenye App ukapewa majibu sasa wakati tunatumia teknolojia aina hii tuwe macho kwanza kujiridhisha lwamba majibu tulioletewa ni sahihi "amesema na kuongeza
"Lakini pia vijana wetu,watumishi wetu na wa Tanzania wasiache kutumia uwepo wao wenyewe binafsi wa akili kutafiti kama jinsi ambavyo enzi za nyuma tumekua tukifanya"
George Mandepo ni Katibu mtendaji Tume ya kurekebisha sheria Tanzania kwa pamoja na Baadhi ya wajumbe wa Baraza hilo wamesema malengo, umuhimu na matarajio yao kwanza ni kuwashirikisha wafanyakazi katika maamuzi kwa sababu ni sawa la Bunge la wafanyakazi maeneo ya kazi.
Katibu mtendaji Tume ya kurekebisha sheria Tanzania Ndugu George Mandepo
Masuala yote yanayohusiana na taasisi ikiwemo bajeti ,muundo yanajadiliwa kwenye kikao kaka hicho cha Baraza la wafanyakazi
Comments
Post a Comment