ASKARI WATAKIWA KUICHUKIA RUSHWA PWANI




Na. Julieth Ngarabali, Pwani.

Askari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani wametakiwa kuichukia rushwa na kufanya kazi kwa kuheshimu  Sheria za nchi na maadili ya utumishi wa umma wanapotumikia wananchi.

Hayo yamesemwa  Aprili 16, na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Pius Lutumo wakati akizungumza na maafisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali wakati akifanya majumuisho ya ziara yake ya ukaguzi kwa Wilaya zote za Mkoa wa Pwani.




Kamanda Lutumo, ameeleza kuwa jukumu la askari ni kutoa huduma bora kwa wananchi wanaowahudumia na kushindwa kufanya hivyo  husababisha jamii kukosa imani na Jeshi la Polisi. 




Aidha, Kamanda Lutumo amekemea vitendo vyote vyenye viashiria vya rushwa kwa askari Polisi wa Mkoa wa Pwani na ameeleza hatasita kuchukua hatua za kinidhamu kwa askari yeyote atakayebainika kujihusisha na  vitendo vya kuomba au kupokea rushwa badala ya kufanya kazi  kwa mujibu wa Sheria za nchi na maadili kwa watumishi wa umma.



Kadhalika, Askari hao wamekumbushwa kutimiza wajibu wao katika kuchukua hatua kwa mtu yeyote anae vunja sheria pasipokuwa na muhali, hususani kwa madereva wanaoendesha vyombo vya moto kupitia barabara kuu za Mkoa wa Pwani.


Club News Editor - Charles Kusaga

Comments

Popular posts from this blog

RC PWANI AONGOZA WAKAZI PWANI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA

BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJINI LAMPONGEZA MKURUGENZI WAKE KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA SAMBAMBA NA KUONGEZA MAPATO.

RAIS SAMIA ATANGAZA KIBAHA MJINI KUWA MANISAPAA,MBUNGE KOKA AFURAHIA ASEMA KIBAHA ITANG'AA