MBARONI KWA KUMDHALILISHA NA KUMTISHIA PINGU WAZIRI NA MBUNGE MSTAAFU.
- Diwani Mstaafu na Askari Mgambo wakamatwa na Polisi Bagamoyo
- Wapata dhamana, kufikishwa Mahakamani wakati wowote
Na Mwandishi wetu Bagamoyo
Jeshi la Polisi mkoani Pwani limemkamata Diwani mstaafu wa kata ya Kiromo Bagamoyo Hassani Usinga maarufu Wembe pamoja na askari mgambo Abdala Mgeni kwa tuhuma ya kumshambulia kwa maneno makali ,kumdhalilisha na kumtishia kumfunga pingu kama muhalifu Waziri na Mbunge mstaafu jimbo la Bagamoyo Dk. Shukuru Kawambwa hali iliyopelekea taharuki kubwa kwa jamii ndani na nje ya Wilaya hiyo.
Watuhumiwa hao wanadaiwa kutenda kosa hilo Aprili 24 saa
nane mchana na kuonekana kupitia kwenye clip ya video iliyosambaa kwenye
mitandao ya kijamii Aprili 25 ikimuonyesha Waziri na Mbunge mstaafu Dk. Shukuru
Kawambwa na mtu mwingine aitwaye Cathbert Madondola wakishambuliwa kwa maneno
makali,vitisho, dharau na kutishiwa kufungwa pingu na Diwani huyo mstaafu akiwa
na askari mgambo huyo.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani Pius Lutumo
watuhumiwa hao wamekamatwa na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya
upelelezi kukamilika.
Lutumo amebainisha kuwa chanzo cha tukio hilo magari ya mchanga
ya mtuhumiwa kuharibu barabara na mashamba ya watu yakipita kwenda kubeba
mchanga eneo la hilo hali iliyopelekea wananchi kufunga barabara kwa magogo ili
kuzuia uharibifu huo wa barabara usiendelee.
Katika clip ya video iliyokua inasambaa mitandaoni iliambatana
na maneno yaliyosomeka kuwa ‘ Shukuru Kawambwa Waziri wa Miundombnu enzi hizo
sasa ni dalali wa viwanja Bagamoyo na muhalifu wa kawaida (common
criminal)
‘’Jeshi la Polisi linamtaka mtu aliyechukua na kusambaza video hiyo mitandaoni ajisalimishe kituo cha Polisi Bagamoyo mara moja”amesema Kamanda Lutumo
Aidha Jeshi la Polisi Pwani linawataka wananchi kuacha
kujichukulia sheria mkononi wafuate sheria za nchi na kuwatumia viongozi
walionao kutatua matatizo yao.
Comments
Post a Comment