RAIS DK. SAMIA ATOA MSAADA WA VYAKULA KWA WAHANGA WA MAFURIKO RUFIJI NA KIBITI





RAISI wa Jamuhuri ya Muungano Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa msaada binafsi wa Tani 300 za vyakula mbalimbali kwa wahanga wa mafuriko Wilayani Rufiji na Kibiti Mkoani Pwani Mwakilishi wa Rais Innocent Mbilinyi ndiye amekabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge na kutaja vyakula vingine ni Tan 100 za mchele, Maharage tan 100 na Unga tani 100.


Akipokea msaada huo, Kunenge ameshukuru na kusema Rais Dk. Samia. amekuwa akipeleka misaada mbalimbali kutoka Serikalini lakini huu wa safari hii ni msaada binafsi kutoka kwa Rais mwenyewe.
"Mheshimiwa Rais amekuwa akituletea msaada kutoka Serikalini lakini msaada huu tuliopokea leo ni msaada binafsi kutoka kwa Rais mwenyewe " amesema Kunenge.
Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Edward Gowelle amemshukuru na kusema msaada huo utakwenda kuondoa changamoto ya mahitaji ya vyakula kwa wananchi wa Rufiji na Kibiti na kuahidi itawafikia walengwa kama ilivyopangwa.
Wilayani Rufiji na Kibiti Mkoani Pwani kasi ya mafuriko hayo ilianza mwanzoni mwa mwezi Aprili mwakahuu na kwamba kwa sasa kata 12 kati ya 13 zimekumbwa na maafa ya mafuriko hayo yanayodaiwa kusababishwa na mto Rufiji kujaa maji yanayotokana na mvua zinazonyesha.


Club News Editor - Charles Kusaga

Comments

Popular posts from this blog

RC PWANI AONGOZA WAKAZI PWANI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA

BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJINI LAMPONGEZA MKURUGENZI WAKE KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA SAMBAMBA NA KUONGEZA MAPATO.

RAIS SAMIA ATANGAZA KIBAHA MJINI KUWA MANISAPAA,MBUNGE KOKA AFURAHIA ASEMA KIBAHA ITANG'AA