SERIKALI KUTENGENEZA SERA YA UINGIZAJI MAGARI NCHINI, MAGARI MABOVU HAYATARUHUSIWA TENA.
Na Gustaphu Haule, Pwani SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ipo mbioni kutengeneza sera ya magari ambayo itazuia uingizaji wa magari chakavu hapa nchini. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais ,Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo ametoa kauli hiyo Machi 26, 2025 mbele ya Waandishi wa habari mara baada ya kutembelea kiwanda cha kuunganisha magari cha GF Vehicle Assemblers Limited kilichopo Kibaha Mkoani Pwani. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo wa pili kutoka kulia akitembelea kiwanda cha GF Vehicle Assemblers Limited kilichopo Kibaha eneo la Tamco alipotembelea Machi 26,2025 kujionea maendeleo ya kiwanda hicho. Kiwanda hicho kilichopo eneo la Tamco- Kibaha Mjini kinaunganisha magari makubwa ya mizigo aina ya FAW yenye uwezo wa kubeba mzigo tani 30. Akiwa katika kiwanda hicho Profesa Mkumbo, amesema kuwa sasa hivi Tanzania mtu anaruhusiwa kuingiza magari hata kama lina miaka 50. Amesema...