TANZANIA KUSHIRIKI MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA DUNIANI

. Na. Charles Kusaga, PWANI TANZANIA inashiriki Kongamano la tano la Kimataifa la Mashirikiano katika Mapambano Dhidi ya Rushwa. Kongamano hili ni mahusus kwa ajili ya Mamlaka za Kuzuia na Kupambana Rushwa Duniani kubadilishana uzoefu na utaalamu katika jukumu la kuzuia na kupambana na Rushwa. Kongamano hili la siku tano, linahudhuriwa na Mamlaka 219 za Kuzuia na Kupambana na Rushwa kutoka nchi 121 Duniani ikiwemo Tanzania ambapo - Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa wanashiriki. Pamoja na mambo mengine, Kongamano hili lilihusisha Warsha ya Wakuu wa Mamlaka za Kuzuia na Kupambana Rushwa (HIGH LEVEL FORUM) kutoa uzoefu wao wa namna Serikali zinavyofanikiwa kudhibiti Rushwa katika mataifa yao. Maeneo yaliyozungumziwa ni pamoja na Maono ya Ulimwengu (GLOBAL VISION), Mfumo wa Kisheria na Kitaasisi (LEGAL AND INSTITUTIONAL FRAMEWORK), Uendeshaji wa Mtandao wa Kimataifa (GLOBAL NETWORK OPERATIONS) na kujenga Ushirikiano. Kupitia Warsha hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TAK...