TANZANIA KUSHIRIKI MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA DUNIANI
Na. Charles Kusaga, PWANI
TANZANIA inashiriki Kongamano la tano la Kimataifa la Mashirikiano katika Mapambano Dhidi ya Rushwa.
Kongamano hili ni mahusus kwa ajili ya Mamlaka za Kuzuia na Kupambana Rushwa Duniani kubadilishana uzoefu na utaalamu katika jukumu la kuzuia na kupambana na Rushwa.
Kongamano hili la siku tano, linahudhuriwa na Mamlaka 219 za Kuzuia na Kupambana na Rushwa kutoka nchi 121 Duniani ikiwemo Tanzania ambapo - Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa wanashiriki.
Pamoja na mambo mengine, Kongamano hili lilihusisha Warsha ya Wakuu wa Mamlaka za Kuzuia na Kupambana Rushwa (HIGH LEVEL FORUM) kutoa uzoefu wao wa namna Serikali zinavyofanikiwa kudhibiti Rushwa katika mataifa yao.
Maeneo yaliyozungumziwa ni pamoja na Maono ya Ulimwengu (GLOBAL VISION), Mfumo wa Kisheria na Kitaasisi (LEGAL AND INSTITUTIONAL FRAMEWORK), Uendeshaji wa Mtandao wa Kimataifa (GLOBAL NETWORK OPERATIONS) na kujenga Ushirikiano.
Kupitia Warsha hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bw. Crispin Francis Chalamila ametoa uzoefu wa namna ambavyo Mfumo wa Sheria na Kitaasisi nchini Tanzania unawezesha Mapambano Dhidi ya Rushwa kufanikiwa.
Mkurugenzi Mkuu amesema Serikali ya Tanzania imekuwa ikipambana na Rushwa kwa kuimarisha mifumo ya sheria na ya kitaasisi ikiwemo kuanzishwa kwa Divisheni ya Mahakama Kuu inayoshughulikia masuala ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.
Ameyasema hayo akiwasilisha mada kuhusu Kupinga rushwa na mfumo wa kitaasisi na kisheria Tanzania 'ANTI CORRUPTION AND INSTITUTIONAL LEGAL FRAME WORK IN TANZANIA' kwa Wakuu wa Mamlaka za Kuzuia na Kupambana na Rushwa wanaoshiriki Kongamano hili la Tano 'The 5th Global Operational Network of Anti Corruption Law Enforcement Authorities - GlobE Network'.
Kongamano hili linahudhuriwa na Mamlaka 219 za Kuzuia na Kupambana na Rushwa kutoka nchi 121 Duniani - Tanzania ikiwa ni kati ya Nchi 70 zilizopewa fursa ya kutoa wasilisho.
Mtandao wa GlobE ulianzishwa 2021 kwa lengo la kubadilishana taarifa, uzoefu na utaalamu katika mapambano dhidi ya Rushwa na TAKUKURU ilijiunga na Mtandao huu Mwaka 2022.
KATIKA HATUA NYINGINE, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bw. Crispin Francis Chalamila, amemtembelea Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Khamis Mussa Omar Septemba 23, 2024 kwa lengo la kujitambulisha.
Akimkaribisha Mkurugenzi Mkuu, Balozi Omar ameipongeza TAKUKURU kwa jitihada inazozifanya katika kuzuia na kupambana na rushwa na kuisisitiza TAKUKURU kutumia vema fursa ya ushirikiano uliopo kati ya Serikali ya Tanzania na ya China kwani kuna mambo mengi ya kujifunza.
Mkurugenzi Mkuu yuko Beijing China kuhudhuria 'The 5th GlobE Network Meeting' inayofanyika Septemba 24 - 27, 2024 ambapo pamoja na mambo mengine amewasilisha mada kuhusu *Mfumo wa Sheria wa Tanzania kwenye Mapambano dhidi ya Rushwa.
Vilevile, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bw. Crispin Francis Chalamila ametumia mkutano huu kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa baadhi ya Mamlaka za Kuzuia na Kupambana na Rushwa wanaoshiriki Mkutano wa GlobE Network unaoendelea Jijini Beijing China kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya TAKUKURU na Mamlaka hizo.
Viongozi aliokutana nao ni kutoka National Commission of Supervision ya China Beijing (NCS), Independent Commission Against Corruption (ICAC) ya China Hong Kong na National Prosecutions Authority - (NPA) ya Afrika Kusini.
Mazungumzo ya Mkurugenzi Mkuu na viongozi hawa yamelenga maeneo yafuatayo:








Kwa ujumla wake viongozi hao wamepongeza jitihada za TAKUKURU katika Kuzuia na Kupambana na Rushwa pamoja na ushirikiano walionao Kikanda na Kimataifa na kuahidi kuendeleza ushirikiano huo.
Comments
Post a Comment