MOUNT CALVARY SPOTRS ACADEMY YAIOMBA TFF KUSAIDIA VIFAA VYA MICHEZO, YAPANIA KUIBUA VIPAJI VYA WANAFUNZI WAO

Na. Gustaphu Haule, Pwani

SHULE ya michezo ya Mount Calvary Sports Academy iliyopo Kiluvya kwa Komba  Kata Kibamba Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es Salaam imeliomba Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) kuona namna ya kusaidia vifaa vya michezo katika Shule hiyo.

Kocha wa mpira wa miguu kutoka Shule ya mchepuo wa michezo Mount Calvary Sports Academy Christopher Mjema akiwa na timu ya wanafunzi wa darasa la Saba na timu ya madarasa ya chini katika mchezo uliopigwa juzi shuleni hapo .

Aidha, mbali na kuiomba TFF lakini pia uongozi wa Shule hiyo imewaomba wadau na wafadhili mbalimbali kujitokeza katika kusaidia changamoto za kimichezo katika Shule hiyo.

Meneja wa Shule hiyo Erick Kilonzo, akizungumza na mwandishi wa habari katika mahafali ya darasa la Saba yaliyofanyika Shuleni hapo hivi karibuni ambapo amesema kuwa shule hiyo imesajiliwa rasmi kuwa kituo cha michezo ya aina mbalimbali.

Kilonzo, amesema kuwa kwakuwa kituo hicho ni kipya kwa Sekta ya michezo ni wazi kuwa zipo changamoto za ukosefu wa vifaa vya michezo ikiwemo jezi,mipira ,viatu na hata miundombinu ya viwanja kwani viwanja vilivyopo vinahitaji maboresho.

Amesema kuwa, lengo la kuanzisha kituo cha michezo shuleni hapo ni kukuza vipaji vya wanafunzi wanaosoma shuleni hapo ambapo amewaomba wazazi kuhakikisha watoto wenye vipaji wanapelekwa Shuleni hapo 

Kilonzo, ameongeza kuwa mtoto ambaye ametokea katika familia yenye kipato duni atapata nafasi ya kuibuliwa kipaji chake bure bila malipo na wale ambao wanataka kusoma basi malipo yake mengine yatabebwa na shule.

Mhadhiri wa chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Frida Ilomo mwenye skafu kulia akiwa na viongozi wa Shule ya Mount Calvary Sports Academy pamoja na timu ya wanafunzi wa darasa la Saba katika mchezo wao uliopigwa Kwa kuwakutanisha wanafunzi wa madarasa ya chini katika Shule hiyo 

"Watoto wenye vipaji ambao hawana uwezo wa kifedha tunawachukua na kuwasomesha bure au kwa kulipa nusu ya ada kwakuwa malengo yetu ni kusaidia katika kuibua vipaji vya michezo kwa wanafunzi.

Kilonzo, ameongeza kuwa kwasasa tayari wamempa Mwalimu wa michezo mwenye sifa na vigezo aliyefundisha timu kubwa Christopher Mjema ambaye tayari ameshaanza kazi ya kutekeleza jukumu hilo.

"Mount Calvary Sports Academy tumemwajiri Christopher Mjema kuwa Mwalimu wa michezo (Kocha) katika Shule yetu  na tunaimani kwa uzoefu wake tutafika mbali katika michezo hasa katika kuibua vipaji kwa wanafunzi wetu na hata vijana wengine wanajifunza michezo hapa Shuleni,"amesema Kilonzo.

Kwa upande wake Mwalimu wa michezo wa Shule hiyo Christopher Mjema, amesema kuwa ratiba ya michezo shuleni hapo ipo sawa kwani hakuna muingiliano wa masomo na michezo ambapo kwa wiki michezo hufanyika mara mbili mpaka tatu .

Kocha wa michezo katika Shule Mount Calvary Sports Academy Christopher Mjema (katikati) akimueleza Mhadhiri wa chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Frida Ilomo juu ya umuhimu wa kutoa vyeti kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika mpira wa miguu shuleni hapo 

Mjema amesema kazi yake kubwa ni kuibua vipaji vya mpira wa miguu na michezo mingine na kwamba michezo hiyo inaanza kufundishwa tangu wanafunzi wa awali mpaka darasa la Saba.

"Nawakaribisha wazazi kuleta wanafunzi wao hapa Mount Calvary Sports Academy kwani mtoto akija hapa anapata faida ya kuibuliwa kipaji chake na faida nyingine ni kufundishwa darasani na walimu wenye uzoefu mkubwa," amesema Mjema

Mjema mbali na kuwa Kocha wa michezo lakini hapo awali ameshawai kuwa Katibu wa Chama Cha Mpira wa Miguu Wilaya Kibaha (Kibaha) , mwenyekiti kamati ya mashindano Chama Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (Corefa) na nafasi mbalimbali za michezo.

Hatahivyo, kutokana na hali hiyo Mhadhiri wa chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Frida Ilomo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo amesema changamoto ya vifaa vya michezo ameichukua na atakwenda kuifanyiakazi 

Kocha wa mpira wa miguu katika Shule ya Mount Calvary Sports Academy iliyopo Kiluvya kwa Komba Ubungo Jijini Dar es Salaam Christopher Mjema akimuongoza Mhadhiri wa chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Frida Ilomo pamoja na viongozi wa Shule hiyo kukagua timu za michezo za Shule hiyo katika mahafali ya darasa la Saba yaliyofanyika Shuleni hapo juzi

Ilomo, amesema kuwa ifikapo mwaka 2025 vifaa vingi vya michezo vitakuwa vimepatikana shuleni hapo huku akiomba wafadhili wengine kujitokeza.

Club News Editor

Comments

Popular posts from this blog

RC PWANI AONGOZA WAKAZI PWANI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA

BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJINI LAMPONGEZA MKURUGENZI WAKE KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA SAMBAMBA NA KUONGEZA MAPATO.

RAIS SAMIA ATANGAZA KIBAHA MJINI KUWA MANISAPAA,MBUNGE KOKA AFURAHIA ASEMA KIBAHA ITANG'AA