DR.CHAKOU TINDWA AKAGUA JENGO LA KITEGA UCHUMI CCM MKOA WA PWANI, AELEZA KURIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WAKE



Na. Gustaphu Haule, Pwani

MJUMBE wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Pwani na makamu mwenyekiti wa Kamati ya uchumi ya CCM Mkoa Pwani Dr.Chakou Tindwa amefanya ziara maalum ya kutembelea na kukagua mradi wa jengo la kitega uchumi la CCM Mkoa wa Pwani.

Dr.Tindwa amefanya ziara hiyo leo Septamba 13 katika jengo hilo lililopo Kibaha Mjini ambapo pamoja na mambo mengine ameeleza kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa jengo hilo .

Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Pwani na makamu mwenyekiti wa kamati ya uchumi Dr.Chakou Tindwa akikagua jengo la kitega uchumi la Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani katika ziara yake aliyoifanya leo Septemba 13.2024.

Akiwa katika jengo hilo Dr .Tindwa amesema kuwa anatamani kuona jengo hilo linakamilika mapema ili kusudi kukisaidia chama kuondokana na usumbufu wa kutumia fedha nyingi kukodi kumbi za watu wengine Kwa ajili ya kufanyia mikutano ya Chama.

"Mimi ni makamu mwenyekiti wa kamati ya uchumi ya CCM Mkoa wa Pwani, hivyo niliona ni vyema leo nikafika hapa kwa ajili ya kukagua jengo hili na kuona maendeleo yake lakini hatahivyo nimeridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa jengo letu,"amesema Dr.Tindwa.

Dr.Tindwa amesema kuwa pamoja na kuchangia fedha kiasi cha Sh.milioni 120 katika harambee iliyofanyika hivi karibuni Jijini Dar es Salaam lakini pia kama kutakuwa na uhitaji mwingine atakuwa tayari kuchangia ili kusudi jengo hilo liweze kukamilika kama iliyokusudiwa.

Mjumbe wa kamati ya Sisa ya Chama Cha Mapinduzi ( CCM) Mkoa wa Pwani na makamu mwenyekiti wa kamati ya uchumi mkoa Dr.Chakou Tindwa akiwa katika jengo la kitega uchumi la CCM Mkoa wa Pwani leo Septemba 13, 2024.

Amewaomba, viongozi wa CCM pamoja na wadau wengine wa maendeleo kuendelea kushirikiana kwa ajili ya kuhakikisha Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani kinapata miradi mingi zaidi ambayo itasaidia kuondoa utegemezi .

Aidha , mwishoni mwa wiki iliyopita Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Ally Hapo,alitembelea jengo hilo na kusifu jitihada za kamati ya Siasa Mkoa wa Pwani kwa kubuni mradi ambao utakuwa na manufaa kwa chama.

Ziara ya Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Ally Hapi katika jengo la kitega uchumi la CCM Mkoa wa Pwani aliyoifanya hivi karibuni.

Hapo, amesema kama kila Mkoa kutakuwa na majengo kama hayo ni wazi kuwa CCM itakuwa imara zaidi ambapo ametaka mikoa mingine kuiga mfano huo.

Club News Editor

Comments

Popular posts from this blog

RC PWANI AONGOZA WAKAZI PWANI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA

BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJINI LAMPONGEZA MKURUGENZI WAKE KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA SAMBAMBA NA KUONGEZA MAPATO.

RAIS SAMIA ATANGAZA KIBAHA MJINI KUWA MANISAPAA,MBUNGE KOKA AFURAHIA ASEMA KIBAHA ITANG'AA