ASASI ZA KIRAIA ZAOMBWA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA SERIKALI.
Na Gustaphu Haule,Pwani KAIMU Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Nsajigwa George, amezitaka asasi za kiraia na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni, uwazi na uwajibikaji ili kuongeza tija katika utoaji wa huduma kwa jamii. Nsajigwa ametoa kauli hiyo Juni 26, 2025 wakati akifungua mkutano wa jukwaa la mashirika yasiyo ya kiserikali mkoa wa Pwani uliofanyika katika Ukumbi wa mdogo wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Pwani. Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani George Nsajigwa akizungumza katika kikao cha mashirika yasiyo ya kiserikali Juni 26,2025 Mjini Kibaha Katika hotuba yake Nsajigwa amesisitiza umuhimu wa mashirika hayo kuzingatia taratibu za kisheria katika utekelezaji wa majukumu yao hasa katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye mchakato wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025. “Mwaka 2025 ni mwaka wa uchaguzi, naomba niagize kuwa mashirika yote yafanye kazi kwa kuzingatia sheria na kanuni,msibadilike na kuwa sehemu ya migawanyiko ya kis...