DKT.CHARLES MWAMAJA AIPIGA TAFU KLABU YA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA PWANI.



Na Gustaphu Haule, Pwani

MDAU wa maendeleo na mkazi wa Kibaha Mjini Mkoani Pwani Dkt.Charles Mwamaja ameipiga tafu Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Pwani kwa kuwapa samani za ofisi ikiwemo viti.

Mwamaja, ambaye pia ni Kamishna kutoka Wizara ya fedha amekabidhi vifaa hivyo Juni 24, 2025 kupitia mwakilishi wake Philemon Maliga hafla ambayo imefanyika katika ofisi za Waandishi wa habari zilizopo Kibaha Mjini.

Picha za makabidhiano ya samani za ofisi baina ya mdau wa maendeleo Dkt.Charles Mwamaja na Klabu ya Waandishi wa habari wa Mkoa wa Pwani.

Awali, akizungumza kabla ya kukabidhi samani hizo  Maliga amesema kuwa  samani hizo ni sehemu ya kuonyesha ushirikiano kati ya Klabu ya waandishi wa habari na wadau wa maendeleo.

 Maliga amesema  kuwa Waandishi wa Habari ni chombo ambacho kinachotumika kuelimisha jamii katika mambo mbalimbali hivyo wanatakiwa kupewa ushirikiano kutatua vikwazo vyao.

Maliga, ameongeza kuwa msaada wa  samani hizo sio mwisho kwani ataendelea kushirikiana na Waandishi wa habari katika kutatua changomto nyingine kwakuwa anaamini waandishi wa habari ndio sauti ya jamii.

"Waandishi wa habari ni chombo muhimu kinachotakiwa kuhabarisha jamii katika masuala mbalimbali yanayohusu   jamii kwahiyo mdau wa maendeleo Dkt.Charles Mwamaja amaeona namna ambayo mnafanyakazi katika mazingira magumu hivyo akaona alete viti ili muweze kufanyakazi katika mazingira mazuri," amesema Maliga.

Mwenyekiti wa klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Pwani Harold Shemsanga amemshukuru mdau huyo kwa kutoa msaada huo ambao unakwenda kupunguza changmoto iliyokuwepo ofisini hapo.
Hafla ya makabidhiano ya samani za ofisi za Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Pwani kutoka kwa mdau wa maendeleo Dkt.Charles Mwamaja iliyofanyika Juni 24,2025 Mjini Kibaha.

 "Mdau huyu wa maendeleo aliona uhaba tuliokuwa nao na kuridhia kutusaidia tunamshukuru kwa moyo wake tunaomba asichoke kutusaidia kwa mara nyingine kutokana na uhitaji ambao bado tunao," amesema.

Shemsanga, amesema kuwa Dkt.Mwamaja ameguswa kwa namna yake na changamoto za Waandishi wa habari na kuamua kusaidia kwa haraka na kwamba mchango wake ni mkubwa na utakwenda kurahisisha utendaji kazi wa Waandishi wa habari.

Aidha, Shemsanga ameahidi kutoa ushirikiano mkubwa  kwa mdau huyo pamoja na  jamii kiujumla na kwamba Waandishi wa habari wapo tayari kufanyakazi kwa ajili ya kusaidia Umma katika kuhabarisha mambo mbalimbali.

Hatahivyo,Shemsanga amesema changamoto katika ofisi hiyo bado hazijaisha na mahitaji yake ni makubwa ambapo ametumia nafasi hiyo kuwaomba wadau wengine kujitokeza zaidi katika kusaidia Klabu hiyo .


Club News Editor

Comments

Popular posts from this blog

RC PWANI AONGOZA WAKAZI PWANI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA

BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJINI LAMPONGEZA MKURUGENZI WAKE KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA SAMBAMBA NA KUONGEZA MAPATO.

RAIS SAMIA ATANGAZA KIBAHA MJINI KUWA MANISAPAA,MBUNGE KOKA AFURAHIA ASEMA KIBAHA ITANG'AA