TAIFA GAS TANZANIA YAMUUNGA MKONO RAIS SAMIA KAMPENI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA


Na Gustaphu Haule, Pwani 
KAMPUNI ya Taifa Gas Tanzania Limited imeendelea kuunga mkono kampeni ya Nishati Safi ya Kupikia ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa elimu na kuhamasisha  wananchi juu ya matumizi ya gas ya kupikia inayouzwa na Taifa Gas. Hii ni Gesi ya Petroli iliyoyeyushwa "Liquefied Petroleum Gas"  (LPG).

 Taifa Gas Tanzania imetoa elimu hiyo leo Juni 7, 2025 katika eneo la Loliondo katika Manispaa ya Kibaha Mkoani Pwani  ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya Nishati Safi Duniani (Gas).

Baadhi ya wananchi wa Kibaha Loliondo wakipata elimu juu ya matumizi ya nishati Safi ya kupikia kutoka kwa wafanyakazi wa Taifa Gas Tanzania ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya siku ya gesi Duniani.

Meneja Uhusiano na Masoko kutoka Taifa Gas Kitengo cha Nishati Safi Anjellah Bhoke ameongoza kampeni hiyo ambapo amesema lengo la Taifa Gas ni kuhakikisha  wanaendelea kumuunga mkono Rais Samia juu ya matumizi ya nishati Safi hapa nchini.

"Leo tupo hapa Kibaha kuhamasisha Wananchi juu ya matumizi ya nishati Safi hususani gesi ya LPG kutoka Taifa Gas na tunapowahamasisha tunatoa mitungi kwa bei nafuu (Promotion) ili kusudi kila Mwananchi aweze kumudu kuinunua,"amesema BHoke

Afisa Uhusiano na Masoko Kitengo cha Nishati Safi kutoka kampuni ya Taifa Gas Tanzania Anjellah Bhoke akitoa elimu ya matumizi ya nishati Safi kwa Wananchi wa Kibaha Mkoani Pwani Juni 7,2025 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Nishati Safi (Gesi) Duniani

Aidha, Bhoke amesema kuwa tangu Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan aanzishe kampeni ya matumizi ya nishati Safi mwaka 2022  kampuni ya Taifa Gas Tanzania ilipokea na kuanza kuifanyiakazi ambapo mpaka sasa mafanikio yake ni makubwa.

Amesema kuwa, mpaka sasa Taifa Gas imewafikia Watanzania wengi waliopo katika Mikoa mbalimbali ambapo kwasasa wanatumia Nishati Safi ya kupikia lakini hatahivyo bado wanaendelea kutoa elimu ili kuhakikisha kila mtu anatumia Nishati Safi.

Wafanyakazi wa Taifa Gas Tanzania wakitoa elimu ya matumizi ya nishati Safi ya kupikia Kwa Wananchi wa Kibaha Loliondo Juni 7 ,2025 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya  Nishati Safi Duniani .

"Taifa Gas imefanya kampeni ya kuhamasisha Watanzania juu ya matumizi ya nishati Safi nchi nzima na sasa nimeona Watanzania wengi wamekubali na kuelewa umuhimu wa matumizi ya nishati Safi lakini sisi kama Taifa Gas bado tunaendelea na kampeni hiyo ili kuwafikia watu wote nchini,"ameongeza Bhoke

Bhoke, amemshukuru Rais Dkt .Samia Suluhu Hassan kwa kuanzisha kampeni hiyo muhimu ambayo inalenga kulinda na kuhifadhi mazingira sambamba na kutokomeza changamoto ya magonjwa yanayotokana na matumizi ya Kuni na Mkaa.

Hatahivyo, Bhoke amewaomba Watanzania kutumia gesi ya LPG kutoka Taifa Gas kwakuwa inauzwa kwa bei nafuu kulingana na mahitaji ya mtumiaji lakini  ni Safi na salama kwa matumizi.

Mtaalamu wa gesi ya LPG kutoka kampuni ya Taifa Gas Tanzania Limited Ambwene Mwakalinga akifafanua umuhimu wa matumizi ya nishati Safi ya gesi kwa Wananchi wa Kibaha Mkoani Juni 7,2025

Kwa upande wake mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Machinjioni Aidan Saimon ameishukuru kampuni ya Taifa Gas Tanzania kwa kufanya kampeni ya kuhamasisha Wananchi wake juu ya matumizi ya nishati Safi.

Saimon,amesema kampeni hiyo imekuja wakati sahihi  kwakuwa matumizi ya Kuni na Mkaa kwasasa hayana nafasi huku akiwasisitiza Wananchi wa Mtaa wake kutumia Nishati Safi ya kupikia hasa inayotokana na LPG kwakuwa ni rafiki wa mazingira.

Club News Editor - Charles Amani

Comments

Popular posts from this blog

RC PWANI AONGOZA WAKAZI PWANI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA

BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJINI LAMPONGEZA MKURUGENZI WAKE KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA SAMBAMBA NA KUONGEZA MAPATO.

RAIS SAMIA ATANGAZA KIBAHA MJINI KUWA MANISAPAA,MBUNGE KOKA AFURAHIA ASEMA KIBAHA ITANG'AA