MAKAMU MWENYEKITI UWT TAIFA ARIDHISHWA UJENZI SHULE YA ENGLISH MEDIUM KATA YA SOFU
Na Gustaphu Haule, Pwani
Club News Editor
MAKAMU mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania ( UWT) Zainabu Shomari ameeleza kuridhishwa na ujenzi wa mradi wa Shule ya awali na Msingi ya Mwalimu Nyerere unaotekelezwa katika Kata ya Sofu Halmashauri ya Mji Kibaha.
Makamu mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Zainabu Shomari akisaini kitabu cha wageni katika Shule ya mchepuo wa Kiingereza ya awali na Msingi ya Mwalimu Nyerere iliyopo Kata ya Sofu Manispaa ya Kibaha alipokwenda kwa ajili ya kukagua Shule hiyo Juni 15,2025.
Makamu mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Zainabu Shomari akisaini kitabu cha wageni katika Shule ya mchepuo wa Kiingereza ya awali na Msingi ya Mwalimu Nyerere iliyopo Kata ya Sofu Manispaa ya Kibaha alipokwenda kwa ajili ya kukagua Shule hiyo Juni 15,2025.
Mradi huo wa Shule yenye mchepuo wa kiingereza unatekelezwa na Halmashauri ya Mji Kibaha kwa fedha za makusanyo ya mapato ya ndani zaidi ya Sh .milioni 700 kupitia force account kwa awamu tatu.
Shomari, ameridhishwa na mradi huo katika ziara yake aliyoifanya Shuleni hapo Juni 15,2025 ikiwa ni sehemu ya kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi ( CCM) katika kipindi cha mwaka 2020 / 2025.
Akizungumza na Wananchi, walimu na baadhi ya viongozi wa CCM wa Kata ya Sofu,Shomari amesema kuwa mradi huo utakuwa chachu ya kusukuma maendeleo ya elimu katika Mji wa Kibaha na hivyo kuwafanya watoto kusoma kisasa.
Amesema kuwa, Serikali imewekeza katika elimu na ndio maana leo Kibaha imepata Shule za mfumo wa Kiingereza na kwamba watoto watapata elimu bila tatizo hivyo wazazi wahakikishe watoto wao wanasoma.
Baadhi ya Wananchi,walimu na viongozi wa CCM Kata ya Sofu wakimsikiliza Makamu mwenyekiti wa UWT Taifa Zainabu Shomari alipotembelea na kukagua mradi wa Shule ya awali na Msingi ya mchepuo wa Kiingereza unaotekelezwa na Manispaa ya Kibaha Mjini kwa fedha za makusanyo ya mapato ya ndani.
"Binafsi nimekuja hapa kukagua mradi huu ili nijiridhishe lakini nasema ukweli mimi nimeridhishwa sana ,ila tunatakiwa kujua Serikali imewekeza fedha nyingi katika mradi huu hivyo wazazi hakikisheni mnazingatia elimu kwa watoto," amesema Shomari
Shomari, amesema kuwa mpaka sasa amepita katika Kata 1098 nchini na kila Kata alikopita amekuta alama ya maendeleo aliyoiweka Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Aidha, Shomari amewaomba Wananchi wa Kibaha Mjini kuendelea kumuunga mkono Rais Samia kwakuwa kazi aliyoifanya ndani ya miaka minne ni kubwa huku akisema imani yake kuwa Rais Samia akipewa miaka mitano ijayo spidi ya maendeleo itakuwa kubwa.
Amesema kuwa baada ya kifo cha Hayati John Magufuli Dkt .Samia alichukua Kijiti japo kulikuwa na taharuki kubwa na wengi walisema hatoweza lakini ameweza kufanya makubwa kiasi ambacho kinawashangaza wengi.
Amesema kuwa, Rais Samia alipoingia madarakani aliikuta miradi mikubwa ya Kimkakati ukiwemo mradi wa Reli ya Mwendokasi (SGR) ambapo wengi walisema hatoweza kukamilisha.
Shomari ameongeza mradi mwingine ni wa Bwawa la kufua umeme la Mwalimu Nyerere na mradi mkubwa wa daraja la Bugongo - Busisi ambapo miradi yote imekamalika huku daraja hilo linalotarajia kuzinduliwa Juni 19,2025 na Rais Samia.
Amesema kutokana na kazi kubwa zilizofanywa na Rais Samia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeona Rais huyo anafaa kuendelea kulitumikia Taifa kwa miaka mitano ijayo na ndio maana chama kimepitisha jina lake kikanuni kuwa mgombea pekee wa nafasi ya Urais .
Shomari amewaomba wanawake wa UWT pamoja na wanaCCM kwa ujumla na Wananchi kuendelea kumuunga mkono Rais Samia kwakuwa mpaka sasa hadaiwi kitu ila yeye ndiye anayedai.
Makamu mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania ( UWT) Zainabu Shomari akikagua Shule ya awali na Msingi ya Mwalimu Nyerere iliyopo Kata ya Sofu Kibaha Mjini katika ziara yake aliyoifanya Juni 15,2025.
Msimamizi wa Shule hiyo Jasmine Msuya, amesema kuwa Shule hiyo ya mchepuo wa kiingereza ikikamilika itakuwa Shule ya tatu Kibaha Mjini ikiwemo Mkoani iliyopo Kata ya Tumbi na Mtakuja Kata ya Pangani.
Msuya, amesema kuwa ujenzi wa Shule ya awali na Msingi ya Mwalimu Nyerere unatekelezwa kwa awamu tatu ambapo awamu ya kwanza imegharimu zaidi ya Sh.milioni 458.
Amesema awamu hiyo ya kwanza imehusisha jengo la utawala, vyumba tisa vya madarasa,matundu 17 ya vyoo,kichomeo taka,ununuzi wa madawati,na samani za ofisi.
Baadhi ya majengo ya Shule ya awali na Msingi yenye mchepuo wa Kiingereza iliyopo Kata ya Sofu Manispaa ya Kibaha Mjini Mkoani Pwani iliyojengwa kwa mapato ya ndani ya Manispaa hiyo.
Msuya, amesema kuwa awamu ya pili imehusisha jengo la maktaba na Tehama, ujenzi wa tenki la ardhini ,mnara wa tenki,ununuzi wa miundombinu ya michezo ya watoto,vitabu, kompyuta
na projekta ambapo imelenga kutumika zaidi ya Sh.milioni 157 lakini mpaka sasa milioni 97 zimetumika na ujenzi umefikia asilimia 85.
Hatahivyo, Msuya amesema kuwa awamu tatu itahusisha ujenzi wa uzio na uwanja wa michezo ambapo inakadiriwa kutumika zaidi ya Sh.milioni 89.
Comments
Post a Comment