WAZAZI PWANI WAPEWA NASAHA ULINZI NA MALEZI YA WATOTO KUNUSURU UKATILI WA KIJINSIA


Na Gustaphu Haule, Pwani 

KAIMU katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali Watu kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Peter Billa amewataka Wazazi, Walezi na Jamii kwa ujumla kuwa walizi wa watoto ili kuhakikisha mtoto anakuwa katika mazingira bora.
Katibu Tawala msaidizi Utawala na Raslimali watu wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Pwani Peter Billa akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika Juni 16,2025 katika viwanja vya Shule ya Msingi Kambarage iliyopo Kata ya Tumbi Kibaha Mjini.

Billa ameyasema hayo leo Juni 16, 2025 kwa niaba ya katibu ya Katibu Tawala Mkoa wa Pwani Rashid Mchatta wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika ambayo kimkoa yamefanyika katika Shule ya Msingi Kambarage iliyopo kata ya Tumbi, Kibaha Mkoani Pwani.

Wanafunzi wa Shule mbalimbali za Msingi wakiwa katika maandamano ya siku ya Maadhimisho ya Mtoto wa Afrika ambapo kwa Mkoa wa Pwani yamefanyika katika Shule ya Msingi Kambarage iliyopo Kata ya Tumbi Kibaha Mjini.

"Yote yaliyoongelewa hapa ni muhimu sana kwa watoto wetu ila niseme tu mtoto anahitaji ulinzi, mtoto anahitaji kulindwa na kuhakikisha anaishi katika mazingira bora, ni wajibu wetu wazazi, walezi, na jamii kuhakikisha hilo", amesema Billa.

Aidha, Billa amesisitiza wazazi kuepuka migogoro ambayo sio ya lazima na kugombana mbele ya watoto kwa kutumia lugha za matusi na vitisho ili kuepuka kuharibu saikolojia ya watoto ambayo itapelekea kufanya vibaya katika masomo yake.

Amesema kuwa, wazazi wanatakiwa kukaa karibu na watoto wao kwa ajili ya kuwasikiliza changamoto zao na kisha kuwatimizia mahitaji yao ya kila siku huku akisema endapo mzazi atakuwa karibu na watoto wao itasaidia kudhibiti baadhi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia Kwa watoto wao.

Katibu Tawala msaidizi wa  uchumi na raslimali watu Peter Billa ,akiwapokea watoto katika Maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yaliyofanyika Kimkoa katika Shule Kambarage Kata ya Tumbi Mkoani Pwani Leo Juni 16,2025.

Billa amewahimiza wazazi pamoja na watoto kushiriki katika ibada na kuepuka kujishughulisha na mambo ya mitaani hali ambayo itapelekea hofu katika kushiriki masuala ya ukatili na vitendo vibaya katika jamii.

Kwa upande wake afisa maendeleo ya Jamii wa Mkoa wa Pwani Grace Tete amesema kilele cha maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika kilitanguliwa na shughuli mbalimbali za kuelimisha jamii kuhusu haki za watoto na waliweza kuwafikia wazazi/walezi zaidi ya 2000 kwa kutembelea maeneo ya masoko mbalimbali yaliyopo Mkoa wa Pwani.

Aidha,Tete amesema kuwa  serikali kupitia mpango wa Taifa wa kuzuia ukatili umetekelezwa na jumla ya watoto 150 waliofanyiwa ukatili wameweza kufikiwa  na kupatiwa huduma stahiki.

Pia alisisitiza wajibu wa Wazazi, Walezi na Jamii kwa ujumla kutimiza mahitaji ya Msingi ya watoto hasa malazi, elimu ,matibabu na chakula  ili kuwawezesha watoto wasiweze kushawishika kirahisi.

Wanafunzi katika maandamano ya Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika Juni 16,2025 katika Shule ya Msingi Kambarage iliyopo Kata ya Tumbi  Kibaha Mjini Mkoani Pwani .

Ameiomba  jamii kumlinda  mtoto dhidi ya  vitendo vya kikatili kuanzia anapotoka nyumbani na kusisitiza  kuimarishwa zaidi kwa mawasiliano kati ya mtoto na mzazi au mlezi ili kuweza kuwa karibu hali itayorahisisha kutambua changamoto zinazowakabili watoto hususan ukatili wa kijinsia.

Naye katika wa CCM kata ya Tumbi Lubawa akizungumza kwa niaba ya diwani wa kata ya Tumbi amewashukuru polisi kata kwa kuimarisha ulinzi na kukabiliana  na masuala mbalimbali ya ubakaji na ukatili wa kijinsia kwa watoto.

Kwa upande wao watoto kupitia maonesho mbalimbali waliyoyafanya kama vile onesho la Bunge, Ngonjera, Shairi pamoja na Risala waliomba utekelezaji wa majukumu kwa wazazi dhidi yao, kuepuka migogoro ya kifamilia pamoja na matumizi mabaya ya mitandao dhidi ya watoto.

Mwisho

Club News Editor

Comments

Popular posts from this blog

RC PWANI AONGOZA WAKAZI PWANI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA

BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJINI LAMPONGEZA MKURUGENZI WAKE KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA SAMBAMBA NA KUONGEZA MAPATO.

RAIS SAMIA ATANGAZA KIBAHA MJINI KUWA MANISAPAA,MBUNGE KOKA AFURAHIA ASEMA KIBAHA ITANG'AA