Posts

Showing posts from April, 2025

MAPATO YA USHURU WA HUDUMA YAPAA KWA KASI KIBAHA MJINI KUTOKA MIL 420 YA MWAKA 2024 MPAKA BILIONI 1.4 YA MWAKA 2025

Image
Na Gustaphu Haule, Pwani  HALMASHAURI ya Mji Kibaha chini ya Mkurugenzi wake Dkt.Rogers Shemwelekwa imefanikiwa kupandisha mapato yatokanayo na ushuru  wa huduma (Service Levy) kutoka Sh.milioni 420 mpaka kufikia Sh.bilioni 1.4. Ongezeko la mapato hayo ni katika kipindi cha mwaka mmoja ikiwa ni kuanzia  Machi 2024 hadi Aprili 2025. Taarifa ya ukusanyaji wa mapato hayo imetolewa na mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Dkt.Shemwelekwa katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichoketi leo Aprili 29,2025 kikilenga kubainisha mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha mwaka 2020)2025. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Dkt.Rogers Shemwelekwa (Pichani)akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichoketi Aprili 29,2025 katika Ukumbi wa Kibaha Shopping Mall. Kikao hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Kibaha Shopping Mall licha ya kuhudhuriwa na Madiwani hao lakini pia kiliwashirikisha watumishi mbalimbali wakiwemo Watendaji Kata na walimu. Wafanyakazi wa kada mbalimbali kat...

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWATAKA WANAHABARI KUONYESHA MAHITAJI YA SERA YA AKILI MNEMBA

Image
Na Gustaphu Haule  WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali imeanzisha mchakato wa kuandaa Sera ya Akili Mnemba, ili kuhakikisha teknolojia hiyo inaendana na misingi ya uhuru wa vyombo vya habari, uwazi na uadilifu katika taaluma ya uandishi wa habari, na kuwataka Waandishi wa Habari kuonyesha mahitaji ya sera ya Akili Mnemba (Akili Unde).  Katika hotuba yake Majaliwa aliyohutubia jijini Arusha Aprili 29, 2025, wakati akifungua maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani (World Press Freedom Day 2025) ambapo kauli mbiu kwa mwaka huu inasema “Uhabarishaji katika Dunia Mpya: Mchango wa Akili Mnemba kwenye Uhuru wa Vyombo vya Habari”.  Amesema kuwa, Serikali inaendelea kupitia upya Sera ya Habari na Utangazaji ya mwaka 2003 ili kuhakikisha inaimarisha na kulinda taaluma ya uandishi wa habari nchini.  “Hivyo, kupitia mijadala yenu katika maadhimisho haya, toeni maoni yenu kuhusu namna sera hiyo ya Akili Mnemba inavyopaswa kuwa ili iendane na mising...

BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJINI LAMPONGEZA MKURUGENZI WAKE KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA SAMBAMBA NA KUONGEZA MAPATO.

Image
Na Gustaphu Haule,Pwani BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Mji Kibaha limempongeza mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Dkt.Rogers Shemwelekwa kwa usimamizi mzuri katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Shemwelekwa ameshushiwa pongezi hizo Aprili 29, 2025 katika kikao cha Baraza hilo kilichofanyika katika Ukumbi wa soko kubwa la kisasa (Kibaha Shopping Mall) ambapo kwa kiasi kikubwa lilikuwa Baraza za kuonyesha mafanikio katika kipindi cha mwaka 2020/2025. Pongezi hizo zilikuja mara baada ya Wenyeviti wa kamati mbalimbali ikiwemo kamati ya fedha, kamati ya Mipango Miji, kamati ya Afya na Elimu pamoja na kamati ya huduma za jamii kueleza mafanikio ndani ya kipindi hicho cha miaka mitano. Mwenyekiti wa kamati ya fedha Karim Ntambo,amesema kuwa katika kipindi cha miaka mitano Manispaa ya Kibaha Mjini imepata mafanikio makubwa ambapo moja ya mafanikio hayo ni pamoja na ongezeko la mapato. Ntambo, amesema kuwa wakati wanaingia madarakani ukusanyaji mapato ulikuwa ni kiasi cha Sh.bilioni 4 la...

MNEC HAMOUD JUMAA AMTAJA SILVESTRY KOKA KUWA MBUNGE HODARI WA UTEKELEZAJI ILANI YA CCM

Image
Na Gustaphu Haule, Pwani  MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi ( CCM) Taifa ( MNEC) Hamoud Jumaa amemtaja Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka kuwa ni mmoja kati ya wabunge vinara na hodari waliotekeleza vizuri ilani ya CCM katika majimbo yao. Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Hamoud Jumaa (MNEC) katikati mwenye shati la njano akiwa pamoja na Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka na Kulia kwake ni mwenyekiti wa CCM Kibaha Mjini Mwajuma Nyamka katika mkutano Mkuu maalum wa Jimbo la Kibaha Mjini uliofanyika Aprili 26,2025. Jumaa, amesema ametembea katika majimbo mengi hapa nchini lakini akijaribu kufananisha anaona Jimbo la Kibaha Mjini kuna kazi kubwa imefanyika na maendeleo zaidi yanaonekana kupitia Koka. Jumaa, ametoa kauli hiyo Aprili 26, 2025 wakati akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu maalum wa Jimbo la Kibaha Mjini ukiwa ni sehemu ya  kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM katika kipindi cha mwaka 202...

SPIKA WA BUNGE DKT.TULIA ACKSON AWAANGUKIA WATANZANIA KUULINDA MUUNGANO KWAKUWA NDIO KIELELEZO CHA AMANI NA UTULIVU

Image
Na Gustaphu Haule, Pwani  SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson amewataka Watanzania kuendelea kuulinda Muungano wa Tanzania kwakuwa ndio kielelezo cha amani na utulivu. Dkt. Ackson ambaye pia ni Rais wa 31 wa Jumuiya ya mabunge duniani ametoa kauli hiyo Aprili 25 wakati akizungumza na viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), viongozi wa Serikali pamoja na wananchi katika katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya Kibaha Shopping Mall.  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo Aprili 25 katika viwanja vya soko kubwa la Kisasa ( Kibaha Shopping Mall); lililopo katika Manispaa ya Kibaha Mjini baada ya kutembelea kiwanda cha Tanzania Biotech Products Ltd na kukagua mradi wa soko hilo. Dkt.Tulia amefanya ziara hiyo katika Manispaa ya Kibaha Mjini ikiwa ni sehemu ya kuelekea katika Maadhimisho ya Siku ya  Muungano wa Tanzania yatakayofanyika Aprili 26, 2025 ...

CPA MAKALLA AWAOMBA WATANZANIA KUSIMAMA NA RAIS SAMIA

Image
Na Gustaphu Haule, Pwani KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi, Siasa na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) CPA  Amos Makalla, amewaomba Watanzania kuhakikisha wanasimama na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025. Makalla, ametoa kauli hiyo Aprili 23, 2025 wakati akifungua mkutano mkuu maalum wa Jimbo la Kibaha Mjini lililopo Mkoani Pwani uliokuwa unahusu uwasilishaji wa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM kwa kipindi cha mwaka 2020/2025 chini ya mbunge Silvestry Koka.   Makalla, amesema kuwa Rais Samia ni kiongozi mahiri na mpenda maendeleo ambaye toka aingie madarakani amekuwa Rais wa kwanza kuvunja rekodi ya kutoa fedha za miradi ya maendeleo kuliko awamu zote zilizopita. "Nawaomba Watanzania wasimame na Dkt.Samia Suluhu Hassan maana amevunja rekodi ya kuwa Rais wa kwanza kutoa fedha nyingi za utekelezaji wa miradi ya maendeleo kuliko awamu zote zilizopita," amesema Makalla  Makalla, amesema Rais Samia amefanyakazi kubwa ya kuiletea maendeleo Tan...

DKT.BITEKO AWATAKA WATANZANIA KUTOGAWANYIKA WAKATI WA UCHAGUZI MKUU

Image
Na Gustaphu Haule  NAIBU Waziri Mkuu Dkt. Doto Biteko amewataka wananchi kutogawanywa kwa itikadi ya dini, ukabila na siasa katika kipindi cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Ubunge na Udiwani. Dkt. Biteko amesema hayo Aprili 23, 2025 Wilayani Monduli mkoani Arusha wakati akizungumza na wananchi mara baada ya kuzindua mradi wa maji katika Kijiji cha Esilalei. “ Ninatamani kuona hatugawanywi na mtu yoyote wala hatuwekwi kwenye makundi ya dini wala ukabila,kwahiyo niwaombe wananchi wa Monduli pendaneni na shirikianeni na uchaguzi utakapofika chaguaneni kwa haki,” amesema Dkt. Biteko. Amewataka wananchi wa Monduli kuutunza mradi huo wa maji wa Esilalei huku akiipongeza Wizara ya Maji na RUWASA kwa kusimamia mradi huo mzuri na wa uhakika. Pia, Dkt. Biteko amesema kuwa Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inawapenda wananchi wa Monduli na inawapongeza kwa uchapakazi wao kwenye kilimo na ufugaji. Aidha, amewataka wachape kazi na kuwa Rais Samia amefikisha mradi h...

CPA AMOS MAKALLA : VIONGOZI ACHENI KUWABEBA WAGOMBEA MIFUKONI MKEKA UTACHANIKA

Image
Na Gustaphu Haule,Pwani KATIBU wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi ( CCM),CPA Amos Makalla amewapiga marufuku viongozi wa chama wanaowahakikishia ushindi watia nia wa ubunge na udiwani kuacha maramoja tabia hiyo kwakuwa wao sio waamuzi wa mwisho. Aidha, Makalla amezitaka kamati za Siasa za Wilaya na Mkoa kuacha kubeba wagombea wao mfukoni kwakuwa kufanya hivyo kunachangia kuwanyima haki wanachama wengine wenye nia ya kugombea katika nafasi hizo. Makalla ametoa kauli hiyo wakati akifungua mkutano mkuu maalum wa Jimbo la Kibaha Mjini uliofanyika April 23, 2025 juu ya uwasilishaji wa taarifa ya utekelezaji wa ilani katika kipindi cha mwaka 2020 / 2025 chini ya mbunge wa Jimbo  la Kibaha Mjini Silvestry Koka.  CPA Amos Makalla Katibu  wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi ( CCM) akisalimia wajumbe wa Mkutano Amesema kuwa, wapo viongozi wanatembea na orodha ya wagombea wa ubunge na udiwani huku wakiwahakikishia kuingia katika tatu bora ambapo am...